Wednesday, April 16, 2014

WAZIRI WA NISHATI UINGEREZA ATEMBELEA SINGIDA, AAHIDI USHIRIKIANO ILI KULETA UMEME WA UPEPO.


Wa kwanza Kushoto ni Naibu Waziri wa Nishati na Madini Stephen Masele, anayefuatia ni Waziri wa Nishati na Mabadiliko ya Hali ya Hewa wa Uingereza Gregory Barker, Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt.Parseko Kone na Balozi wa Uingereza Nchini Dianna Melrose.

Waziri wa Nishati na Mabadiliko ya Hali ya Hewa wa Uingereza Gregory Barker  amefanya ziara ya siku moja katika Mkoa wa Singida akiwa pamoja na Balozi wa Uingereza nchini Dianna Melrose ili kutembelea mradi wa Umeme wa upepo unaoratibiwa na kampuni ya Wind East Africa.
 
Waziri Barker amepokelewa na Wenyeji wake Naibu Waziri wa Nishati na Madini Stephen Masele pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt.Parseko Kone na k
uahidi kushirikiana katika kufanikisha Mradi wa Umeme wa Upepo Mkoani Singida.

Waziri amesema mradi wa umeme wa upepo Mkoani Singida utaunufaisha Mkoa na Nchi kwa ujumla pia uzalishaji wa umeme wa upepo ni rafiki wa Mazingira.  

 Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Parseko Kone akiwa pamoja na Waziri Barker

Kwa upande wake Meneja wa kampuni ya Wind East Africa Rashid Shamte amesema mradi wa umeme wa upepo ambao umewekwa katika eneo la Kisaki Manispaa ya Singida utaanza kuzalisha umeme ifikapo mwaka 2016.

Shamte ameushukuru uongozi wa Mkoa na uongozi wa kijiji cha Kisaki kwa ushirikiano wao ili kufanikisha mradi huo na kuongeza kuwa wananchi wanaona jitihada zao na hivyo kusubiri kukamilika kwa mradi huo wa umeme wa upepo.

Waziri Barker akiwasalimia baadhi ya Viongozi wa  Mkoa wa Singida mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Mjini Singida.

Waziri Barker akiwapiga picha watoto pembezoni mwa uwanja wa ndege wa Mjini Singida.

No comments:

Post a Comment