Akizungumza wakati wa mapokezi ya ugeni huo, Mkuu wa Wilaya ya Singida, Mhe. Godwin Gondwe, akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mhe. HalimaDendego, amesema ugeni huo upo mkoani Singida kwa ajili ya kujifunza masuala mbalimbali yanayohusu usalama, ikiwemo usalama wa chakula, shughuli za uzalishaji kupitia ujasiriamali na viwanda vikubwa, kilimo, ufugaji, ajira kwa vijana pamoja na fursa mbalimbali za kiuchumi.
Mhe. Gondwe ameongeza kuwa ziara hiyo pia imemulika mchango wa lugha ya Kiswahili kama mhimili mkuu wa amani, umoja na ushirikiano unaowaunganisha Watanzania. Aidha, amebainisha kuwa Mkoa wa Singida kwa sasa unazingatia uzalishaji wa mafuta ya kula ya kutosha ili kuunga mkono ajenda ya kitaifa, sambamba na kuweka mikakati bora ya kuwawezesha wajasiriamali wadogo wadogo sambamba na kuwajengea vijana misingi ya kujituma na kuipenda nchi yao.
Mkuu wa Msafara huo, Mkuu wa Chuo cha Ukamanda na Unadhimu Tanzania, Meja Jenerali Steven Mkande, ameeleza kuwa ziara hiyo inalenga kuwajengea uwezo wanafunzi na wakufunzi katika upangaji wa mikakati na mipango ya kijeshi, kwani programu za masuala ya kijeshi zinahusiana moja kwa moja na ulinzi na usalama wa Taifa.
Jenerali Mkande amefafanua kuwa kaulimbiu ya mafunzo hayo kwa mwaka huu inalenga maendeleo ya kiuchumi kwa ajili ya usalama wa taifa, na ziara hiyo ni sehemu ya mafunzo ya vitendo kwani wataweza kutembelea miradi mbalimbali ikiwemo viwanda.
Vilevile ameongeza kuwa, ziara hio inasaidia kupata uelewa mpana wa namna shughuli za kijamii na kiuchumi zinavyoweza kuathiri usalama wa taifa na mazingira, huku wakitathmini fursa zilizopo mkoani Singida kwa kuzingatia idadi ya watu katika sekta za kilimo na ufugaji, pamoja na kuainisha mambo yanayoweza kuathiri usalama kama vile ukosefu wa ajira na umaskini.

Ziara hio ya kimafunzo inatazamiwa kuendelea katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Singida, ikiwa ni sehemu ya mikakati ya chuo hicho cha kijeshi kuwajengea uwezo wa kina maafisa wakufunzi na wanafunzi wa kozi ya ukamanda na unadhimu katika kuunganisha masuala ya maendeleo ya kiuchumi na ulinzi wa amani nchini na duniani kote.

No comments:
Post a Comment