Monday, June 19, 2023

Sitamuelewa Yeyote Atakaye Sababisha Hoja, Upotevu wa Mapato - Serukamba.

Mkuu wa Mkoa Peter Serukamba, leo amelitahadharisha Baraza la Madiwani la Manispaa ya Singida kwamba yupo tayari kuingia kwenye mgogoro na yeyote ambaye atasababisha hoja za CAG kutofungwa, kulegalega kwenye makusanyo na kutofuatilia miradi ya maendeleo.

RC Serukamba ametoa tahadhari hiyo wakati wa Mkutano wa Baraza la maalum la Madiwani la Manispaa ya Singida lililoketi ili kupitia hoja za CAG Mkutano uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Manispaa ambapo zimefungwa hoja 20 kati ya hoja zilizoibuliwa.

RC Serukamba amesema Manispaa  hiyo ina uwezo mkubwa wa mapato ambapo ameeleza kuwa  inaweza kufikia mara mbili ya  fedha zinazokusanywa kwa sasa ambazo ni Milioni 500 kwa mwezi huku akiwataka Madiwani hao kupitia na kusimamia kila chanzo cha mapato ili kufikia malengo yaliyokusudiwa na hatamvumilia yeyote atakayekwamisha makusanyo na kusababisha hoja za ukaguzi.

Aidha, Serukamba ameelekeza kwamba Madiwani washirikiane na wakuu wa Idara ili kufunga hoja zilizobaki na kuhakikisha wanakutana kila mwezi kufanya uangalizi wa mashaka ya kibenki ‘Benk Reconciliation’ ili kuepuka kuzalisha hoja.

Hata hivyo ameagiza kuendela kuboresha hali ya usafi katika maeneo mbalimbali huku akimtaka kutungwa sheria ndogo ambazo zitawabana wanaotupa taka hovyo ikiwa ni pamoja na kutoza faini kubwa jambo ambalo litaongeza mapato ya Manispaa.

Kwa upande wake Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dkt. Fatma Mganga amewataka kuendelea kusimamia miradi ya maendeleo na kuhakikisha hazizalishi hoja.

RAS amewataka kuhakikisha kwamba wanaendelea kupunguza hoja kwa kuzifunga ambapo anaamini kwamba zitapungua hadi kufikia tatu ambazo ni za kisera.

MATUKIO MBALIMBALI KATIKA PICHA

Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba, akizungumza wakati wa Mkutano wa Baraza la maalum la Madiwani la Manispaa ya Singida lililoketi ili kupitia hoja za CAG Mkutano uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Manispaa ambapo zimefungwa hoja 20 kati ya hoja zilizoibuliwa Juni 19, 2023.

Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dkt. Fatma Mganga, akizungumza wakati wa Mkutano wa Baraza la maalum la Madiwani la Manispaa ya Singida lililoketi ili kupitia hoja za CAG Mkutano uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Manispaa ambapo zimefungwa hoja 20 kati ya hoja zilizoibuliwa Juni 19, 2023.

Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa Singida Mhe. Yagi Kiaratu, akizungumza wakati wa Mkutano wa Baraza la maalum la Madiwani la Manispaa ya Singida lililoketi ili kupitia hoja za CAG Mkutano uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Manispaa ambapo zimefungwa hoja 20 kati ya hoja zilizoibuliwa Juni 19, 2023.

Naibu Meya wa Manispaa ya Singida Mhe. Hassan Mkata akizungumza wakati wa Mkutano huo.

Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhandisi Paskas Muragili, akizungumza wakati wa Mkutano huo.

Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Manispaa ya Singida Jeshi Lupembe, akizungumza wakati wa Mkutano huo. 



 Mkaguzi Mkuu wa Mkoa Singida Ofisi ya Mdhibiti na Hesabu za Serikali Othman Jumbe, akizungumza wakati wa Mkutano huo.





No comments:

Post a Comment