Tuesday, February 28, 2023

"Zitumieni VETA kupata Ujuzi" - Chongolo

 

Vijana Mkoani Singida wametakiwa kuepuka kukaa vijiweni badala yake wajiuenge na vyuo vya ufundi stadi VETA ili waongeze ujuzi na waweze kujiajiri na kuitendea haki miradi ya Serikali inayoanzishwa katika maeneo yao.

Kauli hiyo imetolewa leo na Katibu Mkuu CCM Taifa Daniel Chongolo, wakati wa ziara yake ya siku sita Mkoani Singida ambapo alieleza kwamba Serikali imeanzisha vyuo vya ufundi stadi VETA ambavyo vipo karibu kila Wilaya ili viweze kuwasaidia kujifunza na kujiajiri.

Amesema inashangaza kuona miradi ya Serikali inaanzishwa katika Halmashauri mbalimbali lakini wanakosekana vijana wa eneo husika wa kufanya kazi za kiufundi huku wengi wao wakiwa wemejazana vikiwemo.

Hata hivyo Chongolo amebainisha kwamba hakuna ubaya kwa kijana aliyehitimu masomo ya Chuo Kikuu (Degree) na akapata mafunzo ya ufundi stadi ambayo ameleeza kwamba yanamfanya kuongeza ujuzi na kuweza kupambana na kazi yeyote itakayojitokeza.

"Serikali imeanzishwa miradi mingi ya shule, Vituo vya Afya na miradi ya maji lakini nimeshangaa kuona miradi mingine inakwama kwa maelezo kwamba hakuna mafundi, hii ni fursa kila mtu aione na achukue hatua" alisema.

Aidha alieleza kwamba bado Serikali imeendelea kuweka ruzuku katika elimu kupitia programu zake maalum zilizoko chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu ambapo inalipia mafunzo ya ufundi stadi baada ya muhitaji kukamilisha maombi.

No comments:

Post a Comment