Kauli hiyo imetolewa leo na
Mkuu wa Mkoa huo Peter Serukamba alipokutana na Maafisa Elimu na Wakuu
wa Wilaya ili kujadili hali ya usaili wa wanafunzi mashuleni.
Amesema idadi ya Wanafunzi wa Sekondari walioripoti
mashuleni ni ndogo ikilinganishwa na wingi wa madarasa yaliyojengwa na Serikali
hivi karibuni hivyo ni jukumu la Maafisa elimu hao kuhakisha wanasakwa popote
walipo na wapelekwe shuleni.
RC Serukamba ameendelea kueleza kwamba ifikapo Siku ya
Jumatatu tarehe 23 January, 2023 anataka taarifa ya kutoka kila kata kuhusu
wanafunzi wangapi wamesajiliwa na wangapi bado na sababu za kutosajiliwa.
Aidha, ametoa wito kwa wazazi na walezi Mkoani Singida
kuhakikisha hakuna Mtoto aliyechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza
atakayebaki nyumbani.
"Nimejiridhisha kwamba hali ya usaiili wa wanafunzi wa
kidato cha kwanza inasuasua sana, Serikali imejenga madarasa ya kutosha,
imefuta Ada mashuleni lakini bado wapo wazazi hawawapeleki watoto wao shuleni
hili halitakubalika" Serukamba
Kwa upande wake DC wa Iramba Suleimani Mwenda amesema bado
katika Wilaya yake hali ya kujiunga na kidato cha kwanza unaenda kwa kusuasua
jambo ambalo waliamua kuchukua hatua kwa kuwaita wazazi na wanafunzi ofsini
kwake ili kuwasikiliza.
DC Mwenda anasema amebaini kwamba wapo wazazi wanaozuia
watoto kwenda shule ili waweze kujiunga na shughuli za kiuchumi za kulima
kuchunga mifugo na baadhi kutafuta ajira binafsi.
Mwenda amesema wanapenda kutumia mbinu zote zikiwemo
kuwashawishi kutumia Dola kuwapeleka shule na kuwachukulia hatua wazazi watakao
bainika kuwazuia watoto kwenda shule.
Mwisho
No comments:
Post a Comment