Serukamba amaliza mgogoro wa shamba Yulansoni uliodumu
kwa zaidi ya miaka kumi.
Uongozi wa Kijiji cha Yulansoni katika Kata ya Kinyangiri Wilayani
Mkalama Mkoani Singida wameagizwa kuwarejeshea
wakulima mashamba wanayogombania
kwa kuwa hawana vielelezo vya kutosha vinavyoonesha kuwa waliwakodishia wananchi hao mashamba hayo kwa
mikataba.
Agizo hilo limetolewa leo na Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter
Serukamba katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi hiyo baada ya kukutana na viongozi
na wazee wa Kijiji hicho pamoja na uongozi wa Wilaya ya Mkalama.
Amesema yupo mwananchi ambaye ni mjane anayelalamikia
kuzuiliwa kutumia ardhi yake ambayo alifyeka wakati likiwa shamba pori toka
mwaka 1988 lenye jumla ya ekari 65 ambapo viongozi wa kijiji hicho walidai
kwamba walimkodishia kwa mkataba wa miaka nane (8) jambo ambalo RC Serukamba
alitaka Ofisi ya Kijiji kuwasilisha muhutasari wa vikao na mkataba wa makubaliano hayo.
Aidha, Kijiji kiliwasilisha bàadhi ya nyaraka ambazo baadhi
zinaonesha maandishi ambayo yanamtaja mjane huyo badala ya mume wake ambaye
ndio alikuwa mmiliki wa shamba hilo, ambapo
RC Serukamba alisoma nyaraka hizo na kuonekana ziliandikwa mwaka 2005
badala ya 1998 ambapo marehemu ndipo alipofyeka shamba hilo.
Hata hivyo upande wa mlalamikaji uliendelea kudai kwamba
Kijiji hicho kinahitaji shamba hilo ambalo sio mali yake ili kulikodisha ambapo
tayari walishachukua fedha ambapo wanatakiwa akimkabidhi shamba au kurudishiwa
fedha zake.
Kwa upande wake OCD wa Mkalama alikiri kwamba walipata
malalamiko ya mwananchi huyo dhidi ya Kijiji cha Yulansoni ambapo walibaini
mwananchi huyo aliachiwa shamba hilo na marehemu mume wake ambaye naye alipata
kwa kufyeka pori huku Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama Asia Mesos
akieleza kwamba aliwakutanisha mdai na mdaiwa ambapo maelezo ya wote wawili
yanabainisha kwamba mwananchi huyo anamiliki eneo hilo.
Kutokana na maelezo hayo RC Serukamba aliwataka viongozi hao
kuliachia shamba hilo kwa mwananchi huyo aweze kuendeleza shughuli zake za
kilimo na kama hawajaridhishwa na uamuzi huo waende Mahakamani.
Naye Miwani wa Kata ya Kinyangiri Emanuel Kabea alimuomba RC
kutembelea eneo lingine ambalo na lenyewe lina migogoro na Kijiji ambapo
mwananchi aliyefahamika kwa jina la Edward Mnoma alichukua shamba hilo lenye
ukubwa wa ekeri Mia moja (100) ambalo lilikuwa ni eneo la hifadhi ya Msitu wa
Kijiji na akaliuza ambapo kwa sasa limebaki ekari 30 tu.
Aidha Diwani huyo amemuomba RC kutembelea eneo hilo na kuona
kama ekari hizo 30 zilizopo zinaweza
kubaki katika umiliki wa Kijiji hicho jambo ambalo RC Serukamba aliahidi
kutembelea eneo hilo baada ya wiki ijayo kupita.
Wakimalizia mjadala huo viongozi hao wa kijiji walimueleza
Mkuu wa Mkoa huyo kwamba watarejesha shamba hilo kwa mlalamikaji huku
wakijipanga ili kwenda kutafuta haki yao Mahakamani.
Mjadala huo ni muendelezo wa zoezi la utatuzi wa kero za
Wananchi zilizotokana na ziara zake katika Halmashauri zote za Mkoa huo ambapo
aliwasikiliza wananchi kwa kipindi cha Siku nne mfululizo.
Mwisho
No comments:
Post a Comment