Wednesday, January 25, 2023

RC Serukamba atembelea Vituo vya kulisha watoto wanaoishi katika mazingira magumu.

 

Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba amelishauri Shirika la Kimataifa la Outreach linalo hudumia watoto wanaoishi kwenye Mazingira magumu kuendelea kuwapatia huduma ya chakula na misaada mingine hata baada ya kumaliza kidato cha nne mpaka watakapoingia vyuo vikuu kwa kuwa changamoto walizokuwa nazo awali zinakuwa hazijaisha.

Ushauri huo ameutoa leo alipotembelea vituo vya Outreach International vilivyopo Singida mjini na Manyoni lengo likiwa ni kuona miundombinu ya vituo hivyo na namna watoto wanavyopata huduma tarajiwa.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba, akizungumza mara baada ya kuhitimisha ziara yake Wilayani Manyoni kutembelea vituo hivyo vya Shirika la Outreach Internation.

Amelishukuru Shirika hilo kwa kusaidia watoto zaidi ya 1094 ambapo Kituo cha Singida mjini kina idadi ya watoto wapatao 534 na Manyoni 560 kutoka maeneo mbalimbali ambao wamekuwa wakiishi katika mazingira magumu.

Hata hivyo RC Serukamba amepongeza Shirika hilo kwa namna ambavyo wanawapata watoto hao kupitia kwa wenye Viti wa Vijiji na walimu wa shule jambo ambalo ameeleza kwamba watakuwa wanapata watoto wanaoishi kwenye mazingira hayo na sio ubabaishaji.

Kwa upande wake Makamu wa Rais wa Shirika hilo la Outreach Internetional Bw. Mike Wilhelm akitoa maelezo ya awali kwa RC Serukamba amesema kwa sasa wanampango wa kutengeneza vikundi kwa wanafunzi wao waliomaliza kidato cha nne ili kuweza kuwakopesha mitaji kwa ajili ya kufanya  biashara.

Makamu wa Rais wa Shirika la Outreach Internetional Bw. Mike Wilhelm, akitoa taarifa fupi ya Shirika hilo kwa Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba wakati wa ziara yake.

Amesema Shirika hilo mbali ya huduma ya kulisha watoto wamekuwa wakitoa huduma mbalimbali ambapo wameweza kuchimba visima 58 katika Kata ya Ilunda Wilayani Mkalama, Ujenzi wa nyumba 17 za Walimu katika Kata ya Nkungu, mashule na Zahanati katika jamii ya Wahadzabe.

Aidha amesema watoto hao wamekuwa wakifaulu mitihani yao katika mashule wanayotoka kwa asilimia mia moja kutokana na masomo ya ziada wanayofundishwa katika vituo hivyo.

Hata hivyo Mike amesema amelipokea wazo la RC Serukamba na atalifikisha katika Bodi ya Shirika hilo ili kujadiliwa na kufanyiwa maamuzi.

Wanafunzi wakiwa darasani katika kituo cha Outreach International tawi la Singida mjini.



Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba akisani mara baada ya kuwasili katika kituo cha Outreach International tawi la Manyoni mkoani Singida.

Miongoni mwa Watoto wanaopatiwa huduma katika Kituo cha Outreach Internation kilichopo Singida mjini wakiwa katika michezo.




Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba, akizungumza jambo na Moja kati ya Wanafunzi wanaopatiwa huduma katika Kituo cha Outreach International Wilayani Manyoni. Kulia ni Makamu wa Rais wa Shirika hilo.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba, (kushoto) akiwa na Makamu wa Rais wa Shirika la Outreach Internetional Bw. Mike Wilhelm, wakati wa ziara yake Wilayani Manyoni.

Muonekano wa nje katika kituo cha Outreach Internation kilichopo Wilayani Manyoni.

No comments:

Post a Comment