Mkuu huyo wa mkoa wa Singida ametoa kauli hiyo katika
Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi yaliyofanyika Kimkoa wilayani Ikungi Mei 1,
2024 katika viwanja vya standi ya zamani.
RC Dendego, amesema Mabaraza ya wafanyakazi yanafaida kubwa
kwa sababu yanarahisisha kujua changamoto za Wafanyakazi zinazoweza kusababisha
kuzorota kwa ufanisi wa kazi hivyo changamoto zikitafutiwa majawabu mapema
zisaidia wafanyakazi kuongeza bidii na ufanisi kazini.
“Mimi sio Muumini wa Watu wanaovunja Sheria hivyo Waajiri Wakatakao kaidi
Maagizo yangu nitashughulika nao” Amesisitiza RC. Halima Dendego.
Aidha, Mkuu wa mkoa wa Singida ameonya kuhusu Waajiri ambao
hawaruhusu wafanyakazi wao kuanzisha au
kujiunga na Vyama vya Wafanyakazi na kusititiza kuwa jambo hilo ni kinyume cha
taratibu na lazima likomeshwe haraka.
Kuhusu, Madeni ya Wafayakazi Mkoani Singida, Dendego amesema
mkoa huo unaendelea na mchakato wa kulipa madeni ya wafanyakazi na kusema kuwa
Wafanyakazi wa mkoa huo walikuwa wanaidai Serikali zaidi ya Shilingi Bilioni
1.9 na mpaka sasa Serikali imewalipa Wafanyakazi zaidi ya shilingi Milioni 700.
Amesema dhamira ya Serikali ya kulipa madeni ipo pale pale
kinachotakiwa ni uvumilifu tu.
Halima Dendego amewataka Waajiri wahakikishe wanaacha tabia
ya kuzalisha madeni mapya ikiwemo kuhamisha watumishi bila stahiki zao.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa
Shirikisho la Vyama Vya Wafanyakazi Tanzania
( TUCTA) mkoa wa Singida Bi. Agnes Lucas ameishukuru Serikali kwa kuendelea
kulipa madeni ya Wafanyakazi, upandishaji wa madaraja na kuboresha mazingira ya
kufanyia kazi ikiwemo kuwapatia vitendea kazi vya kisasa hali ambayo imesaidia
kuongeza ari na uwajibikaji Sehemu za kazi.
MATUKIO KATIKA PICHA
MENEJIMENTI YA MKOA WA SINGIDA INAWATAKIA HERI YA SIKUKUU YA WAFANYAKAZI 2024
No comments:
Post a Comment