KATIBU Tawala Mkoa wa Singida, Dorothy Mwaluko, ameuagiza
Mradi wa Shule Bora unaotekelezwa katika mikoa tisa (9) nchini kutengeneza
mfumo wa kutoa mafunzo kwa walimu wa Mkoa wa Singida ili kuinua viwango vya
elimu mkoani hapa.
Akifungua mkutano wa uhamasishaji wa Programu ya Shule Bora
kwa wasimamizi na wahariri wa vyombo vya habari leo, amesema walimu watakaopewa
mafunzo hayo nao watakwenda kuwafundisha wenzao.
"Kila Halmashauri kuwe na 'trainers' ambapo kutatafutwa
'centre' walimu watakuwa wanakutana na
hivyo wataguswa walimu wengi kwa wakati mmoja na mpango huu uanze mara moja
mwezi Februari mwaka huu," amesema.
Mradi wa Shule Bora umelenga kuiunga mkono Serikali ya
Tanzania katika kuinua kiwango cha elimu jumuishi pamoja na kuweka mazingira
salama ya kujifunzia kwa wanafunzi wa kike na kiume katika shule za Serikali
zilizopo katika mikoa ya Singida,
Dodoma, Simiyu, Tanga, Mara, Rukwa, Katavi, Pwani na mkoa wa Kigoma.
No comments:
Post a Comment