Friday, June 17, 2022

"Singida ni Mji Pekee hapa Nchini kuwa na Maziwa mawili" RC Singida

 MKUU wa Mkoa wa Singida Dk. Binilith Mahenge ameitaka Manispaaya Singida kuhakikisha tunu waliyopewa na Mungu ya maziwa ya Kindai naSingidani yanakuwa na mazingira ya kuvutia uwekezaji ambao utakuwa vyanzo vikuu vya mapato.

Mkuu huyo wa mkoa ametoa wito huo wakati akizungumza kwenyekikao maalum cha madiwani wa Halmashauri hiyo kilichoitishwa kwa ajili yakujadili hoja za mkaguzi na mdhibiti wa hesabu za Serikali kilichofanyikakwenye ukumbi wa maktaba shule ya Mwenge Sekondari mjini Singida.

Amefafanua kwamba mji wa Singida ni mji pekee hapa nchinikuwa na maziwa mawili ambayo yana fukwe nzuri kwa ajili ya kuweka vivutio vyautalii.

Ameongeza kwamba endapo Manispaa itafanya juhudi za makusudikatika kuweka mazingira ya kuvutia uwekezaji wawekezaji wa ndani na nje ya nchiwatakimbilia kuja kuwekeza.

“Wakazi wa makao makuu ya nchi jijini Dodomawakiwemo  watumishi wa umma na wa taasisi mbalimbali zandani  na  nje ya nchi watavutika kuja kupumzika kwenyefukwe za maziwa hayo mawili. Pia maharusi watatumia mapumziko yao kwenye fukweza Singidani na Kindai”, amefafanua zaidi.

Dk. Mahenge amesema ana imani kubwa kwamba kama Manispaa yaSingida itafanikiwa kuvuta uwekezaji kwenye maziwa hayo watakuwa wamepatavyanzo vya uhakika ambavyo vitaongoza kwa kuingiza mapato makubwa.

“Pia niwahimize kutenga maeneo maalumu ya kupaki magari katikaBarabara ya Singida hadi Arusha, Singida Mwanza Singida Dodoma na Singida hadiMbeya. Maeneo hayo yatakuwa ni vyanzo vingine vipya vya mapato ya ndani. Aidha,amewataka waongeze nguvu zaidi katika kukusanya mapato ya ndani”, amesema Dk. Mahenge.

Katika hatua nyingine, Mkuu huyo wa mkoa ametumia fursa hiyokumpongeza Mkurugenzi na wasaidizi wake kwa kupata hati safi katika kipindi cha2021/2022. Vile vile kuwa na hoja chache za mkaguzi na mdhibiti wa hesabu zaSerikali, ikilinganishwa na halmashauri zingine.

Kwa upande wake Mstahiki Meya Manispaa ya Singida, YangiKiaratu, amemhakikishia Mkuu huyo wa mkoa, kuwa yale yote aliyoyasema, kwao nimaagizo hivyo wanaenda kuyafanyia kazi mapema iwezekanavyo.

Aidha, Kiaratu mwanamke wa kwanza kushika nafasi hiyo ya umeyatoka nchi ipate uhuru, alitumia nafasi hiyo kumshukru na kumpongeza Rais SamiaSuluhu Hassani kwa uamuzi wake wa kutoa bajeti ya Serikali ya2022/2023  ambayo imemgusa kila Mtanzania.

“Kupitia bajeti ya 2022/2023, Samia umewaondolea mzigo mzitowazazi/walezi  kulipa ada za shule kidato cha Tano na Sita. Kwa kwelimama kwa kipindi kifupi ameupiga mwingi. Sisi kama wanawake wenzake, jukumulililo mbele yetu ni kuchapa kazi halali kwa nguvu zote.  Ikiwa nikuwaimanisha wananchi kwamba wanawake tunaweza”, alisema Kiaratu.

 

Wakati huo huo, Mkuu wa Wilaya ya Singida, Paskas Muragiliameipongeza Manispaa ya Singida kwa kuwa na hoja 17 tu, za mkaguzi na mdhibitiwa hesabu za Serikali, na kuwataka wazifanyie kazi kwa muda mfupi.

MWISHO.

No comments:

Post a Comment