Wednesday, January 19, 2022

Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Singida leo Januari 19, 2022 imeanza ukaguzi wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa kupitia fedha za UVIKO 19 pamoja na fedha za tozo ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya CCM inayotekelezwa mpaka mwaka 2025.

Akiongoza ziara hiyo Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida  Alhaji. Juma Kilimba  alisema lengo la ziara hiyo ni kukagua hali ya  utekelezaji wa Ilani ya chama kupitia fedha za UVIKO19  ambazo zimetumika katika ujenzi wa vyumba vya madarasa na vituo vya afya sehemu mbalimbali mkoani hapa.

Aidha, akiongea wakati wa ziara hiyo Alhaji Juma Kilimba  ameshukuru viongozi mbalikmbali wa Chama na  Serikali kwa usimamizi  madhubuti wa ujenzi wa vyumba hivyo na kuwakumbusha kwamba walipewa fedha hizo kwa kuwa waliamainiwa na Serikali ili kusimamia maendeleo kwa wananchi jambo ambalo amelitaka kuendelezwa.

Hata hivyo Mwenyekiti huyo akatoa wito kwa wazazi na walezi  kuhakikisha watoto wanakwenda shule kwa kuwa tayari kila shule ina vyumba vya madarasa na madawati ya kutosha huku akiwataka walimu kuongeza juhudi ya kufundisha kwakuwa miundombinu ya elimu imeboreshwa kwa kiasi kikubwa.

Akipongeza Serikali ya awamu ya sita, Alhaji Kilimba amebainisha kwamba imekuwa ikitekeleza kazi zake kwa uwazi zaidi na kwa kasi kubwa huku akitolea mfano wa ujenzi wa miradi ya vyumba vya madarasa  na vituo vya afya ambapo fedha za maendeleo zimekuwa zikija pamoja na maelekezo ya namna ya kuzitumia.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa  Singida Dkt. Binilith Mahenge  amesema Mkoa ulitengewa jumla ya Tsh. Bilioni 13.4 kwa ajili ya elimu msingi ikiwa ni fedha kutokana na mpango wa maendeleo kwa ustawi wa Taifa  na mapambano dhili ya UVIKO 19.

Aidha RC akaendelea kusema kwamba kiasi hicho cha fedha kilitakiwa kujenga jumla ya vyumba vya madarasa 662 ambapo 330 ni vyumba kwa ajili ya Sekondari na 332 kwa ajili ya Msingi  na vituo shikikizi.

Naye mjumbe wa kamati ya siasa ambeye pia ni Mkuu wa wilaya ya Singida Mhandisi Paskasi Muragili amesema katika wilaya yake kulikuwa na miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya Sekondari ya Ntonge, Mandewa, Mrama, Ilongero, ujenzi wa chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) pamoja na nyumba ya mtumishi.

Miradi mingine ambayo inatekelezwa katika Manispaa ya Singida ni ujenzi wa  Barabara kwa kiwango cha Changarawe eneo la kindai, zahanati ya Unyianga na na kikundi cha utengenezaji wa thamani na kuchomelea madirisha alibainisha Mhandisi Muragili.

Aidha Mhandisi Muragili akaendelea kufafanua kwamba  ukiachilia mbali  fedha za UVIKO 19 zilizotumika katika ujenzi wa vyumba hivyo vya madarsa lakini kuna chumba kimoja cha darasa kilichopo katika shule ya Sekondari Mandewa ambacho kilinjengwa mpaka kukamilika kupitia fedha za tozo.

Akitoa taarifa yake Mkuu wa Wilaya  huyo alibainisha kwamba Halmashauri ya Wilaya ya Singida Hospitali ya wilaya hiyo imepokea fedha kiasi cha  Tsh. Bilion 1.14 kwa ajili ya ujenzi wa wodi tatu ambazo ni chumba cha kuhifadhia maiti na nyumba kimoja kwa ajili ya  watumishi na  chumba cha wagonjwa mahututi ambapo ujenzi unaendelea.

Awali akitoa utambulisho kwa viongozi mbalimbali katika msafara huo, Katibu wa CCM Mkoa Singida  Lucy Shee alisema ziara hiyo inafanyika katika wilaya ya Manyoni na Itigi, Singida DC na Singida MC ambapo kesho ziara hiyo itaendela katika wilaya ya Ikungi, Iramba na Mkalama.

MATUKIO BAADHI KATIKA PICHA WAKATI WA ZIARA


Ziara ikiendelea

No comments:

Post a Comment