Wakuu wa Shule za msingi na sekondari mkoani Singida
wametakiwa kusambaza orodha ya wanafunzi waliochaguliwa kwenye Shule zao na
kuwakabidhi viongozi wa Tarafa, Kata, Vijiji na Vitongoji ili viongozi hao
wafuatilie nyumba kwa nyumba wanafunzi ambao wamechaguliwa na hawajaripoti Shuleni.
Akiongea wakati wa ziara ya kutembelea na kujione hali ya
uandikishwaji wa wanafunzi kwa mwaka 2022 katika Shule zilizopo katika Manispaa
ya Mkoa wa Singida RC Singida Dkt. Binilith Mahenge amesema kila mwenye sifa ya
kwenda Shule lazima ihakikishwe kwamba anaripoti.
Amesema toka Shule zimefunguliwa tareh 17 Januari 2022 ni
asilimia 54 ya wanafunzi wote ndio ambao wameweza kuripoti katika Shule
walizopangiwa hivyo kuwataka viongozi wa kata Tarafa na vijiji kushirikiana na
wakuu wa Shule na kuhakikisha kila aliyechaguliwa
anakwenda Shule isipokuwa tu kwa wale ambao wamehamia Shule binafsi.
Hata hivyo ametoa wito kwa wazazi ambao watoto wao bado
hawajaripoti maShule kutumia kipindi cha wiki moja kuhakikisha wanakwenda Shule
kwa sababu tayari masomo yameanza kufundishwa.
“Hakuna sababu ya mtoto yeyote kutokuja Shule kwa sababu
madarasa yapo ya kutosha, madawati na walimu wapo hivyo Rais wa Jamhuri ya muungano alileta fedha za
kutosha ili kuhakikisha hakuna mwanafunzi ambeye atashindewa kwenda Shule hivyo
kila mzazi ahakikishe kwamba mtoto anasoma.” Alisema Rc Mahenge
Aidha, amewataka wanafunzi wote kuhakikisha wanasoma kwa
bidii na kuweza kufaulu mitihani yao na kufikia ndoto zao ili hiyo iwe kama
zawadi ya shukrani kwa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu
Hassani ambeye alitoa fedha kwa ajilili ya ujenzi wa madarasa hayo.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhandisi Paskasi Muragili
akamhakikisha Mkuu wa mkoa kwamba katika kipindi cha wiki moja baada ya
kufungua Shule watafanya msako kwa kila mtoto ambaye hajafika Shuleni kwa kuwa
kila mwanafunzi wa kila kata kwa kuwa kila familia inafahamika.
Amewakumbusha wazazi kuondoa mazoea ya kwamba Shule
zikifunguliwa wiki ya kwanza inatumika kufanya usafi na kupanga madarasa, hali
ambayo kwa sasa amesema haipo kwa kuwa
kila kitu kiliandaliwa na masomo tayari
yamekwisha anza.
Awali akitoa taarifa ya Manispaa Afisa elimu wa Manispaa hiyo
Bwana Jeshi Lupembe amesema jumla ya wanafunzi 3,976 katika Manispaa ya Singida
walichaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza lakini hadi tarehe 17 Januari 2022
ambayo ni siku ya kufungua Shule jumla ya wanafunzi 1,319 ndio walikuwa
wameripoti.
Amesema Bw. Jeshi Lupembe kwamba kiwango hicho cha kuwapokea
wanafunzi wapya ni dalili kwamba kiwango cha usajili kimeongezeka tofauti na
makadirio yao ya awali.
MATUKIO MBALIMBALI KATIKA PICHA
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge akizungumza wakati wa ziara yake ya kutembelea na kujione hali ya uandikishwaji wa wanafunzi kwa mwaka 2022 katika Shule zilizopo katika Manispaa ya Mkoa wa Singida.
Mheshimiwa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Singida Bi. Yagi Kiyaratu (kulia) akizungumza wakati wa ziara hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhandisi Paskasi Muragili akizungumza wakati wa ziara hiyo.
Diwani wa Kata ya Kisaki Manispaa ya Singida Mhe. Moses Shaban Ikaku akizungumza wakati wa ziara hiyo.
Viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali waliyoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge (wa tatu kutoka kushoto) wakati wa ziara hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Singida (katikati) akiwa na Mkuu wa Wilata ya Singida Mhandisi Paskasi Muragili (kushoto) pamoja na Mkuu wa Shule ya Sekondari Mufumbu Mwl. Muungano Shaban Kibayasi wakati wa ziara hiyo.
Wanafunzi wa kidato cha kwanza wakiwa darasani
No comments:
Post a Comment