Tuesday, September 21, 2021

RC Singida Awataka Vijana Kutumia Teknolojia Ya Simu Kutafuta Masoko

 

Mkuu wa Mkoa Singida Dkt. Binilith Mahenge amewataka vijana kutumia teknolojia ya  mitandao ya simu kutafuta masoko ya bidhaa zao badala ya kutegemea Serikali kufanya kila kitu.

Akiongea wakati wa uzinduzi wa  mradi wa ufugaji wa nyuki wa kisasa  katika kanisa la  Anglikana Muhala unaomilikiwa na  vijana wa Wilaya ya Manyoni chini ya shirika la Compassion  International Tanzania Dkt. Mahenge amesema yapo mataifa ambayo yanauitaji mkubwa wa asali, mbuzi  na ng’ombe  lakini hawajaweza kupata kwa utoshelevu kwa kuwa biashara imekuwa haifanyiki ki kamilifu.

Dkt. Mahenge amewataka vijana kuhakikisha kwamba wanatumia simu uwepo wa simu na mitandao ya kijamii kwa lengo la kuuza na kununua bidhaa mbalimbali

Amesema Serikali imetumia fedha nyingi kuwekeza miundombinu mbalimbali  ikiwemo mkongo wa taifa ili kundi la vijana lipate kufaidika  kupata  soko na marifa mapya ya ki biashara.

Aidha amewataka vijana kulinda miundombinu pamoja na miradi wanayotafutiwa na mashirika mbalimbali pamoja na Serikali ili kufikia lengo la kumkomboa kijana na wanakwake kwa ujumla.

Dkt. Mahenge amebainisha kwamba Serikali inatekeleza sharia inayozitaka Halmashuri kutenga asilimia kumi (10%) kwa ajili ya vijana na asilimia 40 % kwa ajili ya wanawake na walemavu hivyo kumtaka Mkurungezi wa Halmashauri ya Manyoni kuhakikisha kwamba asilimia hiyo  inatumika kuendeleza vijana wilayani hapo.

Naye Afisa vijana wa Mkoa wa Singida Bwana Fredrick Ndahani pamoja na kumshukuru Mkuu wa Mkoa kwa kuzindua mradi wa vijana hao na kuwakabizi vitendea kazi mbalimbali vikiwemo Pikipiki  na mizinga  vyenye thamani ya shilingi milioni 80.4 amezishukuru Taasisi za dini kwa kuwajali na kuwasaidia vijana ambao ni nguvu kazi ya taifa.

Hata hivyo Bwana Ndahani amewaomba  viongozi hao kuendelea kutumia rasilimali walizonazo kuendelea kuwasaidia vijana.

Mwisho amewataka vijana kuendela kuwa waaminifu ili waweze  kuaminiwa na kusaidiwa na jamii inayowazunguka.

Aidha mbali ya uzinduzi wa mradi wa vijana hao mkuu wa mkoa ametembelea  mradi wa ujenzi wa zahanati  ya maweni, shule ya msiningi sayuni na shule ya sekondari ya Mlewa.



                                  

No comments:

Post a Comment