Wednesday, September 08, 2021

Makinda awasihi watanzania kutoa ushirikiano wakati wa sensa

Watanzania wametakiwa kutoa ushirikiano wakati wa utekelezaji wa  zoezi la Sensa ya  majaribio kwa mwaka 2021 ya watu na makazi litakalofanyika katika vijiji 13 vya Tanzania bara  katika mikoa ya Kigoma, Singida, Arusha, Dar es salaam, Mwanza, Morogoro, Mtwara, Njombe na Dodoma.

Akizungumza  na wananchi hivi karibuni katika kitongoji cha kijaroda wilaya ya Mkalama mkoani Singida Kamisaa wa Sensa ambaye pia ni spika  mstaafu wa  Bunge  la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Anna Semamba Makinda  amesema sense hiyo ya majaribio itaanza tarehe 08 mpaka 19 mwezi huu hivyo  ushiriki wa wananchi ni muhimu katika  kufanikisha zoezi hilo.

Aidha amesema zoezi la sensa ya majaribio kwa mwaka 2021 litatoa mwelekeo, fursa na changamoto katika  kujipanga na sensa ya mwaka 2022.

“Tukifanya vizuri mwaka huu  itakuwa ni dalili ya kufanya vizuri Zaidi mwaka kesho kwa sababu tutakuwa tumejifunza kutokana na  changamoto za kipindi hiki” alisema Makinda.

Amesema sensa ya mwaka huu itakuwa ni tofauti na vipindi vingine ambayo ilikuwa inaishia katika ngazi ya wilaya na mkoa lakini kwa mwaka huu na mwaka kesho itakuwainafanyika hadi ngazi ya kitongoji.

Lengo la sensa hii ni kutaka kufahamu juu ya makazi majengo, anuani, idadi ya watoto, vijana na wazee ambao wapo ili waweze kuendana na bajeti ya Serikali. Alibainisha mama Makinda.

Aidha mama Makinda amesema sensa ni muhimu kwa taifa kwa sababu itasaidia kusukuma gurudumu la maendeo ya jamii, kusaidia kuratibu uwepo wa miundombinu ya shule, hospitali, barabara, makazi na hata mikopo kwa wanafunzi.

Akimalizia hotuba yake Kamisaa wa sensa Mama Makinda amewatoa hofu wananchi kwamba makarani watakaohusika katika zoezi hilo wamepata mafunzo ya kutosha na wamekula kiapo cha kutunza siri za  watu wakati wa kuhesabu.

Naye mratibu wa sensa katika ngazi ya mkoa wa Singida Bw. Naeng’oya Kipuyo amesema maandalizi ya  sense  mkoani hapo yamekamilika kwa kuwa tayari maeneo yameshatengwa na uhamasishaji umefanyika kwa kiasi kikubwa.

Amebainisha kwamba sensa ya majariibio kwa mkoa wa Singida itafanyika kwa muda wa siku tatu kuanzia tarehe nane (8)   mpaka  10 ambapo wataalamu watangazia huduma za kijamii zinazopatikana  eneo hilo.

Usiku wa tarehe 10 kumkia tarehe 11 itafanyika sensa ya majaribio katika Kitogoji hicho kuhesabu watu waliolala katika nyumba zao zoezi litakalochukua siku tatu (3) mpaka tarehe 13 alibainisha bwana Kipuyo.

Amesema tarehe 14 mpaka 16 zoezi la sensa litaendelea katika Kitogoji hichio cha Kijaroda ambapo itafanyika sensa ya majengo, wamiliki na huduma zinazofanyika katika nyumba hizo na mwisho ilatakuwa  ni kuchukua anuani za makazi kwenye kila nyumba alimalizia bwana Kipuyo.

Mery christiani ni msichana mkazi wa Kitogoji hicho ameishukuru Serikali kwa hatua hiyo na kuwasihi wananchi kutokuwa waoga na kuhakikisha wanajitokeza kuhesabiwa ikiwa ni  pamoja na wenye mahitaji maalumu ili waweze kupata  mahitaji yao ya baadae.

Matukio katika picha

Wananchi wa Kitongoji cha Kijaroda wilayani Mkalama wakifuatilia hotuba ya Kamisaa wa sensa Mhe. Anna Makinda alipotembelea eneo hilo tarehe 7/9/2021 
Mratibu wa sensa mkoa wa Singida Bw. Naeng'ya Kipuyo (kulia) akizungumza wakati wa mkutano na wananchi wa Kitongoji cha Kijaroda 

Mkuu wa wilaya ya Mkalama Mhe. Sophia Mfaume Kizigo (kushoto) akihutubia wananchi kuhusu umuhimu wa sensa ya watu na makazi katika eneo hilo.
Afisa uhamasishaji wa sensa Bw. Andrew Punjila akiwagawia wananchi vipeperushi vya elimu ya sensa na umuhimu wake wakati wa mkutano huo. 

Mkutano ukiendele katika Kitongoji cha Kijaroda

No comments:

Post a Comment