Mkuu wa Mkoa wa Singida Dokta Parseko Vicent Kone akikata utepe wa vitabu na kuzindua mpango mkakati wa kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi na vifo vya watoto.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dokta Parseko Vicent Kone jana amezindua Mpango mkakati wa Mkoa wa kuongeza kasi ya kupunguza vifo vya akinamama vitokanavyo na uzazi na vifo vya watoto.
Dokta amezindua mpango mkakati huo ulioshirikisha wadau wa sekta ya afya na ustawi wa jamii Mkoani Singida ukiwa na kauli mbiu ya, 'Weka kipaumbele, wekeza, timiza wajibu, okoa maisha'.
Amesema licha ya mafanikio katika utoaji wa chanjo, Mkoa bado una kasi ndogo ya kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi na vifo vya watoto akitoa mfano wa mwaka 2011 hadi 2013 vifo vya akinamama vimepungua kutoka 52 hadi 49 na watoto wachanga kutoka 182 hadi 178.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dokta Parseko Vivent Kone.
Aidha Dokta Kone amesema ufuatiliaji wa utekelezaji wa mpango mkakati huo utafanyika kwa njia mbalimbali ikiwepo teknolojia mpya ya kadi rafiki ya kufuatilia huduma za afya ya mama na mtoto.
Ameongeza kuwa mkakati huo utazingatia upimaji wa huduma kabla ya ujauzito na matumizi ya njia za uzazi wa mpango, huduma wakati wa ujauzito, huduma za mama aliyejifungua na mtoto mchanga na unyonyeshaji wa maziwa ya mama katika kipindi cha miezi sita ya kwanza.
Dokta Kone amezitaka halamshauri Mkoani Singida kuandaa ratiba ya utekelezaji wa Mpango mkakati huo na Sekretarieti kuandaa ratiba ya ufuatiliaji na tathmini ili malengo ya mkakati huo yaweze kufikiwa kama yalivyoazimiwa.
Wadau wa sekta ya Afya Mkoani Singida wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Singida Dokta Parseko V. Kone akizindua mpango Mkakati wa Kuongeza kasi ya kupunguza vifo vya akina mama vitokanavyo na uzazi na vifo vya watoto wachanga.
Wadau wa sekta ya Afya
Mkoani Singida wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Singida Dokta Parseko V.
Kone akizindua mpango Mkakati wa Kuongeza kasi ya kupunguza vifo vya akina mama vitokanavyo na uzazi na vifo vya watoto wachanga.
No comments:
Post a Comment