Tuesday, October 21, 2014

KAMPENI YA KITAIFA YA CHANJO YA SURUA-RUBELA YAZINDULIWA MKOANI SINGIDA.






Mkuu wa Mkoa wa Singida Dokta Parseko Vicent Kone amkimpa mtoto matone ya Vitamin A katika uzinduzi wa Chanjo ya Surua-Rubela Mkoani Singida.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dokta Parseko Vicent Kone amewashauri wazazi na walezi kutoamini maneno ya upotoshaji juu ya chanjo ya Surua-Rubela kwakuwa hazina madhara na huimarisha kinga ya mwili dhidi ya magonjwa hayo.

Dokta Kone ametoa rai hiyo jana katika kijiji cha Mlandala kata ya Mwiru Wilaya ya Ikungi wakati akizindua rasmi chanjo ya Surua-Rubela Mkoani Singida.

Amesema chanjo ya Surua-Rubela ina uwezo wa kukinga mwili dhidi ya magonjwa ya surua na rubela ambayo yasipopatiwa matibabu mapema huweza kusababisha vifo na ulemavu kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano.


Mkuu wa Mkoa wa Singida Dokta Parseko Vicent Kone akipokea dawa za matende na mabusha katika uzinduzi wa Chanjo ya Surua-Rubela Mkoani Singida.

Dokta Kone amesema kampeni hiyo ya kitaifa inahusisha utoaji wa matone ya vitamin A kwa watoto wa miezi sita, chanjo mpya ya Surua-Rubela kwa watoto wa umri wa miezi tisa mpaka chini ya miaka 15, dawa za minyoo kwa watu wote kuanzia umri wa mwaka mmoja na dawa za matende na mabusha kwa watu wote kuanzia miaka mitano.

Aidha ametaja baadhi ya madhara ya kutopata chanjo hizo ni pamoja na kuugua magonjwa hayo ambayo huweza kusababisha kifo, upofu, kutokusikia vizuri, utindio wa ubongoi, ulemavu na mama mjamzito akiugua ugonjwa wa rubela anaweza kujifungua mtoto mfu au njiti.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa Dokta Dorothy Gwajima amesema katika kampeni hiyo Mkoa umedhamiria kutoa chanjo kwa watoto  631,139  itakayopatikana katika vituo 199 vilivyoainishwa.

Dokta Gwajima amesema tatizo la magonjwa yanayofanyiwa kampenilipo katika Mkoa wa Singida ambapo mwaka 2013 kulikuwa na wagonjwa matende wanne, mwaka 2014 watu wanne wamegundulika kuwa na surua na mmoja alibainika kuwa na rubela.





















Mganga Mkuu wa Mkoa wa Singida Dokta Dorothy Gwajima akisoma taarifa ya utekelezaji wa kampeni ya kitaifa ya Chanjo ya Surua-Rubela Mkoani Singida.

Mmoja wa wananchi waliohudhuria uzinduzi wa chanjo hiyo Ramadhani Ginza wa Kijiji cha Malandala ametoa ufafanuzi juu ya magonjwa ya matende na mabusha na kuonyesha madhara yake kisha akatoa mfano kwa kuanza kunywa dawa za matende na mabusha.

Ramadhani Ginza akinywa dawa za matende na mabusha katika uzinduzi wa kampeni ya kitaifa ya Chanjo ya Surua-Rubela Mkoani Singida.

























Baadhi ya wananchi waliohudhuria uzinduzi wa kampeni ya kitaifa ya Chanjo ya Surua-Rubela Mkoani Singida.

























Akina mama na watoto wao wakisubiri chanjo katika kituo cha kutolea Chanjo ya Surua-Rubela Mkoani Singida.

No comments:

Post a Comment