Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk. Parseko Vicent Kone.
Watu wawili wamepoteza maisha na wengine
33 kujeruhiwa katika Kijiji cha Nkuhi,wilaya ya Ikungi, mkoani Singida baada ya
basi la Kampuni ya KISBO SAFARY lililokuwa likitokea Dar-es-Salaam kwenda
Kahama kupasuka gurudumu la mbele na kisha kupinduka mara tatu.
Mganga
Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Singida, Dk.Deogratius Banuba amethibitisha kupokea majeruhi na maiti hao na kuongeza kuwa kati ya
majeruhi hao kumi wamevunjika mifupa.
Aidha, mmoja kati ya majeruhi waliolazwa wodi namba tatu katika Hospitali hiyo, Bi Wilhelimina
Stephano amesema tangu walipofika Chalinze basi hilo
lilianza kusumbua kama vile kuna kitu kama mpira uliokuwa ukiungua.
Mkuu
wa Mkoa wa Singida, Dk.Parseko V. Kone ameonyesha masikitiko yake kutokana na ajali hiyo na kukemea
tabia ya baadhi ya madereva wanaokwenda mwendo kasi unaosababisha ajali na vifo
vya abiria.
No comments:
Post a Comment