Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk. Parseko Vicent Kone akikagua moja ya maabara za sekodari za kata Manispaa ya Singida iliyo katika hatua za ukamilishaji.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk. Parseko Vicent Kone amewataka wananchi Mkoani Singida kuchangia ujenzi wa vyumba vitatu vya maabara za fizikia, kemia na biolojia katika sekondari zote za kata kwani elimu bila ya sayansi maendeleo ni hafifu.
Dk. Kone ametoa rai hiyo wakati akikagua ujenzi wa maabara za sekondari za kata za manispaa ya Singida mapema Jumatano na Alhamisi wiki hii.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk. Parseko Vicent Kone akikagua moja ya maabara za sekodari za kata Manispaa ya Singida.
Amesema mabadiliko makubwa duniani ya teknolojia yameletwa na wanasayansi hivyo ujenzi wa maabara hizo utawajengea uwezo wanafunzi wa shule hizo kuwa wanasayansi bora hapo baadae.
Dk Kone ametoa mchango wa zaidi ya shilingi milioni kwa sekondari za Dokta Salmini, Mughanga, Mungumaji, Unyamikumbi, Kisaki, Kimpungua, Ipembe na sekondari ya Mandewa.
Aidha amewataka watendaji na madiwani kuhakikisha kuwa ifikapo Oktoba 15 mwaka huu maabara zote katika sekondari za kata za manispaa ya Singida ziwe zimekamilika.
Dk Kone amewaasa watumishi wa serikali na wale waliochaguliwa na chama cha Mapinduzi (CCM) kushirikiana kwa pamoja ili kufanikisha maendeleo Mkoani hapa.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk. Parseko Vicent Kone akikagua moja ya maabara za sekodari za kata Manispaa ya Singida.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk. Parseko Vicent Kone akikagua moja ya maabaraza sekodari za kata Manispaa ya Singida.
Moja ya maabara za sekodari za kata Manispaa ya Singida zilizo katika hatua ya umaliziaji.
No comments:
Post a Comment