Saturday, September 06, 2014

MKUU WA MKOA AIPONGEZA WILAYA YA MKALAMA KWA HATUA NZURI YA UJENZI WA MAABARA ZA SEKONDARI.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Parseko Kone akisikiliza taarifa ya ujenzi wa maabara ya sekondari ya Ibaga katika chumba kimojawapo cha maabara kilichokamilika na kutumiwa  katika wilaya ya Mkalama.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Parseko V. Kone ameipongeza halmashauri ya wilaya ya Mkalama kwa kuhamasisha ujenzi wa maabara za Sekondari na hivyo kupiga hatua kubwa katika ujenzi huo.

Dkt. Kone ametoa pongezi hizo mwishoni mwa wiki hii mara baada ya kumaliza ziara ya kukagua ujenzi wa maabara katika halmashauri 4  za Manispaa, Singida vijijini, Mkalama na Manyoni.

Amesema wananchi si wagumu katika kuchangia maendeleo isipokuwa viongozi wanapaswa kutoa elimu juu ya michango hiyo na kuwahimiza kushiriki katika shughuli za maendeleo.

Dkt. Kone amesema ujenzi wa maabara za sekondari utasaidia kuongeza wanasayansi nchini ambao ni muhimu katika maendeleo ya nchi.

Amewashauri watendaji kuanzia ngazi ya wilaya, tarafa, kata, vijiji na mitaa kushirikiana ili kufanikisha ujenzi wa maabara kwakuwa ni jukumu la kila mwananchi. 


























Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Parseko Kone akifungua mlango wa maabara ya sekondari ya Mwangeza iliyopo wilaya ya Mkalama.









Jengo la maabara ya sekondari ya Mwangeza iliyopo wilaya ya Mkalama.


























Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Parseko Kone akitoa maelekezo ya ukamilishaji wa maabara ya sekondari ya Shelui iliyoko wilaya ya Iramba.


Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Parseko Kone akipokea taarifa ya ujenzi wa maabara ya sekondari ya New Kiomboi iliyoko wilaya ya Iramba.

No comments:

Post a Comment