WAKANDARASI wazawa wametakiwa wanapopewa zabuni za ujenzi wa miradi wawe wanaikamilisha ndani ya muda wa mkataba ili Serikali iendelee kuwapatia kazi zaidi.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida, Martha Mlata, amesema hayo leo (Julai 25, 2023) baada ya kutembelea mradi wa maji katika Kijiji cha Mughunga Wilaya ya Singida DC akiwa na wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Mkoa.
Wajumbe wa kamati hiyo walipotembelea mradi huo ambao wanakagua utekelezaji wa Ilani walibaini mkandarasi wa kampuni ya Universal Construction Co Ltd aliyepewa zabuni ya ujenzi wa mradi huo hali inayotia wasiwasi huenda asikamilishe Agosti 17, mwaka huu kama mkataba unavyoelekeza.
"Tunapata malalamiko kwamba Serikali haiwapi miradi wakandarasi wazawa na badala yake wanapewa wa nje lakini tunaomba nyie wazawa mnaopewa fanyeni kazi kufa na kupona kuonyesha uaminifu kwa Serikali ili iendelee kutoa zabuni kwa wakandarasi wazawa zaidi lakini mnaposuasua mnakuwa hamuaminiki," amesema.
Naye Meneja wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Lucas Said, alisema mkandarasi wa kampuni hiyo ameshaandikiwa barua ya onyo na iwapo atashindwa kukamilisha mradi ndani ya muda wa mkataba Agosti 17,2023 na maji kuanza kutoka Septemba Mosi mwaka huu atanyang'anywa na hatapewa kazi nyingine tena.
No comments:
Post a Comment