Mkuu wa Mkoa wa Singida. Peter Serukamba ametoa onyo kwa
maafisa ugavi mkoani hapo ambao wamekuwa wakisabisha ucheleweshaji wa
miradi inayotekelezwa kwa ‘force Account’ kwa
kuweka michakato mirefu ya manunuzi ambayo kwa mujibu wa taratibu za
mirad hiyo haihusiki.
Onyo hiyo amelitoa hivi karibuni wakati akikagua miradi ya
ujenzi wa Vituo vya Afya na Shule vilivyopo Wilayani Manyoni Mkoani hapo ambapo
kila alipobaini changamoto yoyote kwenye mradi alitajwa afisa manunuzi kwamba
anaendelea na michakato ya ununuzi jambo ambalo RC Serukamba amesema sio
sahihi.
Amesema miradi inayotumia ‘force account’ huwa zinaundwa
kamati tatu ambazo ni kamati ya manunuzi, ya mapokezi na kamati ya ujenzi
ambazo kila moja inashughulikia na kazi yake hivyo haikuwa na sababu ya maafisa
ugavi kununua, kuingilia au kuratibu michakato ya manunuzi.
"Afisa manunuzi kwenye miradi hii anahusikaje? kuweka
michakato ya ununuzi kwenye miradi hii ni kutupotezea muda na kutafuta faida
kwa upande wake, kamati zilizoteuliwa ki sheria zinatosha"
RC Serukamba alitembelea miradi minne ambayo ni ujenzi wa wodi mbili na mochwari katika
hospitali ya Wilaya hiyo, Kituo cha Afya Sanza,
Ujenzi wa shule ya Msingi Nanduka na shule ya msingi Heka ambapo kati ya
hiyo ni mradi mmoja tu wa Nanduka ambao hajakutana na changamoto ya ucheleweshaji
wa ununuzi wa vifaa vya ujenzi kama mbao na mabati.
Akiwa katika mradi wa ujenzi wa wodi ya wanawake RC
Serukamba ameendelea kusema kwamba hatamuonea aibu yeyote atakayesababisha
fedha za miradi kurudi huku akiendelea kusisitizia kwamba atawachukulia hatua
watakao onekana kuchelewesha mradi kwa hila zao.
MATUKIO KATIKA PICHA
No comments:
Post a Comment