Wakurugenzi wa Halmashauri wameagizwa kuongeza usimamizi wa fedha za mapato kutoka vyanzo mbalimbali na kuhakikisha hakuna mkusanyaji anaye kaa na fedha zaidi ya siku mbili bila kuipeleka benki.
Maagizo hayo ameyatoa
Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba
leo wakati wa kikako cha kamati ya ushauri ya Mkoa (RCC) kilichofanyika
katika ukumbi wa mikutano wa ofisi hiyo ambapo aliwataka Wakurugenzi kueleza
kwa nini mpaka sasa bado kuna wadaiwa (defotars) katika Halmashauri zao.
Aidha amewataka wenyeviti wa Halmashauri kwa kushirikiana na
wakuu wa Wilaya kuhakikisha wote wanaodaiwa wanalipa fedha hizo na ikibidi
hatua zaidi zichukuliwe kwa kuwapeleka Mahakamani au kufuta madeni ambayo
uchunguzi utabaini kukosekana kwa ushahidi.
Amesema maendeleo ya wananchi yanategemea namna ambavyo makusanyo yanavyoongezeka kwa kuwa vinategemeana hivyo kwa kuchelewesha malipo hayo ameelekeza kwamba ni kuwachelewesha wananchi maendeleo.
No comments:
Post a Comment