Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba amewataka Wakurugenzi wa Halmashauri zote Mkoani hapo kufanya tathmini ya mapato yanayopatikana kwenye minada inayofanyika kwenye maeneo yao na kuibinafsisha kwa wafanyabiashara ili kuokoa mapato yanayopotea kwa kuwatumia Watumishi wa Umma katika ukusanyaji.
Akiongea katika Mkutano uliofanyika leo tarehe 04.06.2022 katika ukumbi wa mikutano wa ofisi hiyo Rc Serukamba amesema mapato mengi yanapotea kutokana na uzembe wa wakusanyaji wa mapato hayo.
Amesema minada hiyo inauwezo mkubwa wa kuongeza mapato kwenye Halmashauri lakini makusanyo yapo chini kwakuwa unaomilikiwa na wakuu wa Idara pamoja na Madiwani hivyo kushindwa kudai ushuru kama inavyotakiwa.
Katika kufanikisha zoezi hilo RC Serukamba ametoa wiki moja kwa kila Mkurugenzi awe amefanya utafiti kubaini uhalisia wa mapato kwa kila mnada.
Aidha Mkuu wa Mkoa ameahidi kukutana na wote wanaodaiwa na Halmashauri hizo kwa nyakati tofauti siku ya Jumamosi ya tarehe 09 Octoba, 2022 ili waweze kurejesha fedha hizo ikiwa ni pamoja na kuonana na wenye vibanda katika masoko mbalimbali na wa miliki wa vizimba.
"Kila Mkurugenzi afanye tathimini ya fedha zinazopatikana kwa sasa katika minada, utafiti wangu unaonesha kwamba tunaweza kupata zaidi ya mara mbili ya fedha tunazopata sasa, binafsisheni minada hiyo kwa wafanyabiashara naamini tutapata fedha nyingi zaidi" alisema Serukamba.
Aidha, amewataka Wakurugenzi wa Halmashauri kuandaa mikataba ambayo wataingia na wakusanyaji wa mapato kwenye minada.
Katika hatua nyingine RC Serukamba ameagiza Maafisa ugani wa Halmashauri kuongeza kilimo cha nyanya na vitunguu katika mabonde ili kuongeza biashara ya mazao.
No comments:
Post a Comment