Mamlaka ya Maji Safi na usafi wa Mazingira SUWASA imetakiwa kuweka Mpango mkakati ya kuwa na mifumo ya ukusanyaji maji taka (sewage system) ambayo watayatibu na kuyarudisha tena kwenye matumizi ya kawaida ili kupunguza changamoto ya upatikanaji wa maji katika maeneo mbalimbali ya nchi.
Kauli hiyo imetolewa leo na Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter
Serukamba leo alipokuwa kwenye hafla ya
kushuhudia utiaji saini Mkataba wa Mradi wa Ujenzi wa Mabwawa ya
kutibu majitaka baina ya SUWASA na Mkandarasi M/S Perntels Company and Nangai Engineering and Contractors iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa
Bonde la Kati.
RC Serukamba amesema ujenzi wa mabwawa hayo pamoja na kwamba yatawasaidia wananchi kuendesha shughuli za kilimo lakini bado yanaweza kusaidia upatikanaji wa maji ya uhakika endapo yatatibiwa na kurudi kwenye chanzo cha maji na kuendelea kutumiwa na jamii.
Aidha, amewataka SUWASA kuhakikisha wanaongeza wigo wa
huduma za maji hasa maeneo ya pembezoni mwa miji ili kuondoa changamoto ya upatikanaji wa maji.
Amesema Mradi huo utagharimu kiasi cha Bilioni 1.73 na
utatumia muda wa miezi 18 na utajengwa katika eneo la Manga katika Manispaa ya
Singida.
Hata hivyo RC amewataka wananchi kuwapa ushirikiano mkubwa
Wakala wa maji Safi na usafi wa Mazingira Mkoa wa Singida SUWASA katika kipindi
cha Ujenzi wa Mradi huo ambao utawasaidia kwa kiasi kikubwa hasa katika upatikanaji
wa mazao ya bustani kutokana na uwepo wa maji ya umwagiliaji.
Mwisho
No comments:
Post a Comment