Wananchi Mkoani Singida wametakiwa kutoa ushirikiano mkubwa kwa Makarani na Wasimamizi wa Sensa za watu na makazi ya mwaka 2022 zoezi litakalo anza usiku wa Agosti 23 mwaka huu ili kila mtu aweze kuhesabiwa.
Hayo yamesemwa leo na Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba wakati akifungua Kongamano la wadau wa Sensa lililofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Chuo cha Uhasibu Mkoani hapo.
Amewataka wananchi hao kuhakisha wanajiandaa kuhesabiwa na kuandaa taarifa za kila mmoja huku Mkuu wa Kaya akihakikishia anatoa ushirikiano kwa Makarani wa Sensa ili kuwapatia taarifa hizo.
Aidha Serukamba amewataka viongozi Mkoani hapo kila mtu kwa nafasi yake ahakikishe zoezi hilo linafanikiwa kwa kiwango kikubwa, ikiwa ni pamoja na kuwashirikisha viongozi wa vitongoji na mabalozi ili waweze kuwasadia Makarani kufika maeneo yao ya Utawala.
"Kama mlivyofanya wakati wa anwani za makazi kama mlivyofanya wakati mlipotenga maeneo ya majaribio ya Sensa, basi mkafanye hivyo hivyo wakati wa zoezi la kuhesabu watu. Alisema
Hata hivyo RC Serukamba amewataka viongozi hao wa kisiasa na kijamii kuendelea kuhamasisha wananchi kuhusu umuhimu wa kujitokeza kuhesabiwa na kushirikiana na Makarani wa Sensa watakapokuwa wanafanya kazi yao.
Katibu Tawala Mkoa wa Singida Mwl. Dorothy Mwaluko akizungumza wakati wa kikao hicho
Kwa upande wake Katibu Tawala Mkoa wa Singida Mwl. Dorothy Mwaluko akimkaribisha mgeni rasmi amewataka watendaji kuhakikisha wanafuata maagizo na maelekezo yatakayotolewa katika kikao hicho ili kuboresha zoezi hilo.
Aidha Serikali iliamua kuunda kamati hizo zenye mchanganuo wa Wenyeviti wa Halmashauri, Wakurugenzi watendaji na wakuu wa Wilaya ili kukumbusha wajibu wa kila mmoja katika kutekeleza zoezi la Sensa ya watu na makazi katika maeneo yote ya utendaji na uongozi.
Mratibu wa Sensa Mkoa wa Singida Naing'oya Kipuyo akizungumza wakati wa mkutano na wadau wa Sensa mkoa wa Singida.
Awali akitoa taarifa ya utanguli pamoja na utambulisho Mratibu wa Sensa Mkoa wa Singida Naing'oya Kipuyo amesema fedha zote kwa ajili ya kuwalipa Makarani zilishafika na kutumwa kwenye Halmashauri husika ili waweze kuwalipa Makarani na Wasimamizi katika maeneo yao.
Hata hivyo Kipuyo amesema zoezi la ulipaji limekamilika ambapo mpaka jana usiku Halmashauri zilikuwa zinalipa mkononi "cash" walikuwa wameshamaliza kulipa ila wachache ambao malipo yao yalipitia kwenye mabenki waliendelea kupata.
No comments:
Post a Comment