Friday, August 12, 2022

Mwenge wa Uhuru Watua Singida Mjini watoa Siku tatu kwa Tanesco kuhakikisha Umeme umefika shule ya msingi Mwembe Mmoja.

Shirika la Umeme Nchini Tanesco limepewa na Mwenge wa Uhuru Siku tatu kuhakikisha Umeme umefika katika shule ya msingi Mwembe Mmoja huku Mkurungezi akipewa Siku mbili kukamilisha usukaji wa nyaya za Umeme katika jengo hilo.

Akiongea leo tarehe 12.08.2022 baada ya ukaguzi wa Ujenzi wa shule ya Mwembe Moja na Uwamaka zilizopo katika Manispaa hiyo  yaliyojengwa kwa fedha za miradi ya  Uviko Kaimu Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Emanueli Ndege Chacha amepongeza viwango vya Ujenzi vilivyotumika katika majengo hayo ambapo amewataka Tanesco kuhakikisha wanasogeza Umeme maeneo hayo.

Amesema  kwa kuwa majengo yamekamilika na yameanza kutumika lazima kuwepo na miundombinu itakayoruhusu matumizi ya teknolojia ya kompyuta katika shule hizo mbili.

Aidha Mwenge wa Uhuru umemwelekeza Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Jeshi Lupembe kuhakikisha wanasuka nyaya (wiring) ndani ya siku chache ili Umeme uweze kuingizwa katika majengo hayo.

Hata hivyo Mwenge wa Uhuru umelekeza kwa upande wa Mradi wa shule ya Uwamaka kutumia vyanzo vyake vya ndani ili kukamilisha majengo mawili yaliyo baki.

Akitolea ufafanuzi kuhusu uingizaji wa Umeme katika majengo hayo Meneja wa Tanesco Mkoa wa Singida Muhandisi Florence Mwakasege amesema wapo tayari kutekeleza maagizo hayo na ndani ya Siku tano watakuwa wamekamilisha zoezi hilo huku akimtaka Mkurugenzi kupeleka maombi na malipo kwa ajili ya Mita.

Akimalizia hotuba yake kwa niaba ya Kiongozi wa Mwenge Emanueli Chacha amewataka wananchi wote kujitokeza kuhesabiwa katika SENSA ya Watu na Makazi itakayofanyika tarehe 23.08.2022.

Mwisho 

No comments:

Post a Comment