Tuesday, May 17, 2022

wawili wapoteza maisha kwenye Mgodi wa Senkeke Iramba Mwingine aendelea Kusakwa

 Watu wawili wamepoteza maisha na mmoja akiwa hajulikani alipo kufuatia ajali ya kuzama kwenye maji yalioko ndani ya mgodi kulikosababishwa na kuvunjika kwa chanja iliyokuwa inatengenezwa mgondini hapo ili kutumika Kama daraja la kuvukia upande wa pili.

Wakaguzi wa Mgodi huo wamekiri Kutokea kwa ajali hiyo baada gema lilikuwa limeshikilia chanja hiyo kukatika na kusababisha watu wanne Kati ya Sita walioingia mgondini hapo kuzama majini ambapo watatu Kati yao waliweza kuokolewa kabla ya kupata madhara makubwa.
Hayo yamebainika leo tarehe 16.05.2022 wakati Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt.Binilith Mahenge alipotembelea Mgodi wa senkeke uliopo Wilayani Iramba ambao watu hao wawili walikutwa na umauti na tayari wamekwisha opolewa huku jitihada za Kutafuta mwili wa tatu zikiwa zinaendelea.
Kufuatia ajali hiyo RC Mahenge akiwataka wakaguzi na wasimamizi wa migodi yote Mkoani hapo kuchukua tahadhari za mapema pamoja na kutoa taarifa kwa wakati Kwa mamlaka husika pindi wanapopata changamoto hizo ili kuokoa Maisha ya wafanyakazi wa migodi hiyo.
"Toka tatizo Hilo limetokea imechukua zaidi ya masaa 24 mamlaka hazijapata taarifa
Ambapo zingeweza kusaidia zoezi la uokoaji kwa watu wetu ,Kamishna wa Madini utoaji wenu wa taarifa haukukaa vizuri Nina uhakika Jeshi letu la zimamoto lingesaidia kuokoa watu Hawa lakini hamkuwapa taarifa" alisema RC Mahenge
RC Mahenge ametoa onyo Kali kwa wasimamizi wa migodi ambao hawakukagua usalama wa maeneo ya kazi kabla ya kuingiza wafanyakazi ndani ya mgodi na kumtaka Kamishna wa Madini kushirikiana na vyombo vingine kufanya uchunguzi ili kubaini chanzo Cha tatizo
Aidha Mahenge ameagiza kupitia kwa Kamishana wa Madini Mkoani hapo kuhakikisha kwamba migodi yote inakaguliwa na kuona ubora wake ikiwa ni pamoja na kuwepo kwa vifaa vya uokoaji na kuhakikisha kwamba wakaguzi wa Shughuli za migodi wanawajibika Katika kazi zao ili kuokoa Maisha ya wengine
Hata hivyo RC Mahenge ametoa pole kwa wafiwa wote na kuwapongeza vijana walioshiriki Katika kuopoa miili ya marehemu hao ambao ilikuwa imezama katika maji yaliopo ndani ya mgodi huo na kusisitizia kuimarisha vifaa vya uokoaji na usimamizi
Awali akitoa taarifa Chone Lugangizya Malembo
Kaimu Kamishna wa Madini amesema walioingia ndani ya mgodi walikuwa Sita wakaguzi wawili na wafanyakazi wa mgondini walikuwa wanne ambapo baada ya chanja yao kuvunjika kwa kuangukiwa na gema wakaguzi wawili pamoja na mfanyakazi waliweza kuokolewa huku waengine watatu wakizama ndani ya maji kwa kushindwa kuogelea.
Hata hivyo Kamishana lugangizya amebainisha kwamba bado Kuna uzembe uliofanywa na wakaguzi hao kwa kushindwa kutathmini gema walilotumia kuegeshea chanja hizo kwamba ni imara kiasi gani huku akimhakikishia mkuu wa Mkoa kwamba eneo ajali ilipotokea palikaguliwa na.kuonekana ni miongoni mwa maeneo salama.
Akipokea maelekezo kutoka kwa Mkuu wa Mkoa Chone Lugangizya Malembo amesema wataendelea kutekeleza maagaizo yake huku akibainisha kwamba wamekuwa wakifanya ukaguzi wa migodi yote Mara kwa Mara na kutoa ushauri kwa wahusika Jambo ambalo wataendelea nalo.
Kamishina amewashikuru makampuni mbalimbali pamoja na migodi ambayo imesaidia vifaa na wataalamu wakati wa zoezi la uokoaji vikiwemo pampu za kutolea maji ndani ya mgodi.
Mwisho.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge (kushoto ) akitoa maelekezo kufuatia kupoteza maisha kwa watu wawili na mmoja bado hajapatikana baada ya kuanguka kwenye maji ndani ya mgodi wa Senkeke uliopo wilaya ya Iramba kulia ni kamishina wa madini Chone Lugangizya Malembo baada ya kukutana katika eneo hilo leo
Mkuu wa Mkoa akiangali shimo ambako vija hao walizama ndani na kukutwa na umauti

wakaguzi wa mgodi wa senke ke ( inspectors) wakitoa maelezo kwa njia ya ramani kuhusu ambavyo walikuwa wakijenga chanja ambayo ilishindwa kuhimili na kusababisha vifo vya watu hao wawili.
Mashuhuda na Wafanyakazi wa Mgodi wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Mkoa Binilith Mahenge akitoa Hotuba yake kuhusu usalama wa maeneo ya migodi

No comments:

Post a Comment