Wawekezaji
wa aina mbalimbali wameaswa kuendelea kuwekeza Mkoani Singida kwa kuwa kuna
fursa nyingi za uwekezaji na ni katikati ya nchi jambo ambalo linarahisisha
usafirishaji wa bidhaa kutoka sehemu moja kwenda nyingine.
Miundombinu
ya Barabara mazingira mazuri ya ki
biashara yameendelea kuboreshwa Mkoani hapo ili kuvutia uwekezaji na biashara
kwa ujumla.
Kauli hiyo
imetolewa hivi karibuni na Mkuu wa Mkoa huo Dkt. Binilith Mahenge wakati
akizindua ufunguzi wa duka jipya la vifaa vya Ujenzi lililopo Singida
mjini lijulikanalo kama NAJEL BUILDERS
COMPANY LIMITED.
Dkt. Mahenge
ameipongeza Kampuni hiyo kwa kuwaletea wana Singida huduma hiyo nakubainisha
kwamba usambazaji wa bidhaa hizo za Ujenzi zitanufaisha mikoa yote ya pembezoni.
Aidha
ameitaka Kampuni hiyo kuuza vitu vyenye ubora wa Hali ya juu ili kuwanufaisha
wananchi wa Singida lakini pia kuimarisha soko katika maeneo yote ya ndani na
nje ya Mkoa.
Hata hivyo
amewataka wawekezaji kuendelea kuwekeza kwa kuwa Serikali inaendelea kuboresha
Mazingira ya Biashara ikiwemo kutenga maeneo mahsusi kwa wamachinga
nakuimarisha ulinzi na usalama wa watu na mali zao.
Naye
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Singida Mhe. Yagi Kiaratu amesema uwekezaji kama
huo unafaida kwa Serikali na Manispaa kwa kuwa wanachangia kodi ya mapato
ambayo itaharakisha maendeleo kwa wananchi.
Kwa upande
wake Mkurugenzi wa Kampuni ya NAJEL BUILDERS Ltd Mhandisi Neema Nzwalile
amemshukuru Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Binilith Mahenge kwa kukubali wito huo
sambamba na mapokezi mazuri ya Serikali ya Mkoa huo katika sekta ya uwekezaji
hali iliyoongeza chachu na hamasa kwa wawekezaji wazawa.
Hafla hiyo
ilihudhuriwa na viongozi mbali mbali wakiwemo waheshimiwa Madiwani wa Singida
Mjini, Wahandisi wa Ujenzi kutoka sekta binafsi, mafundi Ujenzi pamoja na
wafanyabiashara wa mkoani Singida.
MATUKIO KATIKA PICHA
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa duka la vifaa vya ujenzi la Kampuni ya Najel Builders LTD mkoani Singida
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge (wa pili kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Waheshimiwa Madiwani wa Singida Mjini, Mkurugenzi wa Kampuni na baadhi ya wageni waalikwa walioshiriki katika uzinduzi huo.
No comments:
Post a Comment