Vyama vya Wafanyakazi, Waajiri pamoja na Takukuru wametakiwa kushirikiana ili kuondoa aina zote za rushwa ikiwemo rushwa ya ngono katika upatikanaji wa ajira mkoani Singida.
Kauli hiyo imetolewa hivi karibuni na Mkuu wa Mkoa huo Dkt. Binilith
Mahenge wakati akihutubia Wafanyakazi kwenye maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi
duniani (Mei mosi) iliyofanyika katika uwanja wa Liti mkoani hapo.
Mkuu wa Mkoa alibainisha hayo wakati akijibu risala ya chama
cha Wafanyakazi mkoani hapo ambapo walibainisha uwepo wa rushwa ya ngono katika
maeneo ya kazi katika zoezi la
upatikanaji wa ajira.
RC Mahenge alisistiza kwamba katika kuadhimisha sikukuu ya
Wafanyakazi mkoani hapo watumishi wanapaswa kuachana na mambo ya rushwa. "Takukuru
nawaagiza mshirikiane na Waajiri pamoja na vyama vya wafanyakazi mkoani hapa
ili kuondoa aina zote za rushwa ambazo zinaonekana pamoja na zile zilizosomwa katika
risala na kiongozi wa vyama vya wafanyakazi mkoani hapa" alisema
RC Mahenge.
Awali Katibu Tawala wa Mkoa huo Dorothy Mwaluko aliwataka Wafanyakazi
kufanya kazi kwa juhudi na maarifa ili kuweza kuwatumikia Wananchi kama
inavyotakikana.
Amesema kudai mishahara na marupurupu kuendane na utekelezaji
wa majukumu yaliyo bora ili kuleta usawa wa vyeo na mishahara kulingana na
mishahara inayotolewa.
"Nimeona Watumishia wa Serikali Mkoani hapa mkicheza
kwaito na mkienda kwa Stepu kwa kupokezana
bila kukosea ikionesha umahiri mlionao Katika mchezo huo, niwaombe Stepu
hizo zitumike Katika kuwahudumia Wananchi
katika ofisi zenu. Alisema Dorothy Mwaluko katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi
duniani
MATUKIO KATIKA PICHA
No comments:
Post a Comment