Ikiwa yamebaki masaa 32 kufikia 48 yaliyotolewa na Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dorothy Mwaluko akizitakaTaasisi zote za Serikali zilizopo mkoani hapo ziwe zimebandikwa anwani za makazi, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo imekuwa ya kwanza kutekeleza agizo.
Akipokea kibao cha anwani ya makazi chenye namba 43102 kutoka Shirika la Posta Mkoa wa Singida
Katibu Tawala huyo amesema ukaguzi wa vibao hivyo utafanyika kama ilivyopangwa
na muda uliowekwa ukikamilika.
"Tuliposema tunatoa masaa 48 vibao viwe vimebandikwa
tulikuwa tunamaanisha hivyo, na Mimi nishatekeleza kuhakikisha kibao
kinapatika na kinabandikwa na huu ndio uwajibikaji ninao utarajia kwa kila Taasisi"
alisema Dorothy Mwaluko
Aidha amewataka wakuu wa Taasisi kuhakikisha wanasimamia zoezi hilo ili likamilike kwa wakati.
No comments:
Post a Comment