Taasisi zote za Serikali mkoani Singida zimepewa masaa 48 kukamilisha uwekaji wa anwani za Makazi katika maeneo yao kama sehemu mfano lengo likiwa ni kuharakishwa ufanikishaji wa zoezi hilo.
Kauli hiyo imetolewa leo na Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dorothy Mwaluko katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi hiyo wakati wakipokea taarifa ya utekelezaji wa uwekaji wa anwani za Makazi katika Halmashauri Saba (7) za Mkoa huo.
Katibu Tawala huyo amezitaka kila Taasisi ya Serikali mkoani hapo kwa kutumia gharama zao ifikapo tarehe 29 April 2022 sawa na masaa 48 kuhakikisha wameweka vibao katika maeneo yao.
Hata hivyo RAS huyo amesema zoezi la uwekaji wa namba katika nyumba na majina ya Mtaa yanatakiwa kukamilika kwa Mkoa mzima kabla ya tarehe tano mwezi Mei mwaka huu na kuwakumbusha Wakurugenzi wa Halmashauri kusimamia kikamilifu zoezi hilo.
Hata hivyo Mwaluko amebainisha kwamba hakuna mgogoro wa ardhi mkoani hapo ambao unaweza kuwa changamoto katika utoaji wa anwani za makazi kwa kuwa vipomo vya aridhi vimebainisha kuwa hakuna migogoro hivyo kuwataka wanaotekeleza zoezi hilo kuacha kutumia migogoro kama kigezo cha kuchelewesha kazi.
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu Wizara ya habari, Mawasiliano na Technolojia ya habari Mohamed Khamisi, amesema Mkoa wa Singida umechelewa kufikia malengo ya uwekaji wa anwani za Makazi hasa katika nyumba na majina ya mitaa hivyo kuwataka wasimamizi kukamilisha zoezi hilo kabla ya Mei tano mwaka huu.
"Nilipotoka Dodoma nilipita katika baadhi ya mitaa kadhaa ya Mkoa wa Singida sikuona vibao vya mitaa wala namba kwenye nyumba, tumechelewa tunatakiwa tukimbie ili tuweze kwenda sawa na mikoa mingine" Katibu Mkuu
Katibu Mkuu huyo akaelekeza kukamilika kazi hiyo mapema kwa kuwa timu itakuja kufanya ukaguzi kabla ya taarifa kukabiziwa kwa Mamlaka nyingine mwishoni mwa mwezi Mei.
Awali akiwasilisha taarifa ya operesheni Anwani za Makazi kwa Mkoa mzima Athuman Simba amesema jumla ya anwani 343,815 zimekusanywa na kusajiliwa kwenye mfumo wa NaPA ikiwa ni sawa na asilimia 103.48
Kikao hichi kilishirikisha Wakurugenzi wa Halmashauri zote za mkoa huo pamoja na waratibu wa zoezi hilo.
No comments:
Post a Comment