Wafanyabiashara
wa vitunguu mkoani Singida leo wamepigwa marufuku kutumia matumizi ya vifungashio ambavyo havijathibitishwa
na Serikali na ambavyo vinazidi kilo mia kwa kuwa vinawapunja wakulima.
Akiongea na
wafanyabiashara katika soko la vitunguu lililopo Kata ya Misuna mkoani hapo
wakati wa zoezi la kufanya usafi Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhandisi Pasksi Muragili
amewataka wafanyabiashara katika soko hilo kuachana na matumizi ya vifungashio ambavyo
havijathibitishwa na Serikali badala yake watumie vifungashio aina ya neti.
Amewataka
viongozi wa Soko hilo kuwachukulia hatua wafanyabiashara wote wanaotumia
vifungashio vyenye ujazo wa magunia unaozidi kilo Mia moja maarufu kama rumbesa
kwa kuwa unawapunja wakulima.
"Serikali
ilishatoka muongozo kuhusu matumizi sahihi ya vifungashio lakini nimepata
taarifa kwamba bado wafanyabiashara wanaendelea kutumia viroba na magunia ambayo
ni zaidi ya kilo Mia naomba kuanzia leo asiwepo mfanyabiashara anayetumia
kifungashio zaidi ya neti ambayo imekubalika. Tunafanya hivi ili kuwasaidia
wakulima wetu" Mhandisi Muragili.
Awali akihutubia
wananchi walioshiriki shughuli za usafi katika soko hilo ikiwa ni sehemu ya
kusherehekea sikukuu ya Muungano amesema zoezi hilo liwe endelevu na kila mtu awe
na kawaida ya kufanya usafi katika maeneo yanayo wazunguka.
Mhandisi
Muragili amebainisha kwamba Mkoa umejipanga kuhakikisha inaongoza kwa usafi
hapa nchini na ndilo dhumuni la kuhakikishia usafi unafanyika kila siku.
Katika
kuhakikisha zoezi linafikia lengo Mhandisi Muragili amemtaka Mkandarasi anayehusika
na uzoaji la taka kuhakikisha wanaondoa vizimba vya taka kabla ya kufikia saa
nae mchana wa leo.
Amesema
anafahamu kwamba Mkandarasi anayesafisha eneo hilo la soko ana vitendea kazi
vingi ikiwemo magari lakini hana vijiko kwa ajili ya kuzolea taka hivyo kumtaka
akatafute ufumbuzi juu ya hilo ili aweze kusaidia kufikia lengo la kuweka Safi
Mkoa.
Alimalizia
hotuba yake DC Muragili akawataka wananchi kushiriki kikamilifu katika zoezi la
utoaji wa chanjo ya polio kwa watoto chini ya umri wa miaka mitano tarehe 28
Aprili 2022.
Amewataka
wananchi kushiriki zoezi hilo na kuwataka kuupuzia uvumi unaosemwa katika
mitandao ya kijamii kwamba chanjo hiyo ina madhara, amesema wataalamu wa afia
wamejiridhisha kwamba chanjo hizo ni salama kwa watumiao na inayoletwa kwa
matone kwa watoto wote waliyopata au ambao hawajapata chanjo hiyo.
Amesema
zoezi la chanjo hiyo limetokana na uwepo wa waathirika wa Polio katika nchiza
jirani hivyo Serikali imeamua kuchukua tahadhari kwa kuwachanja watu wake ili
kuepusha tatizo hilo. Alibainisha DC Muragili.
Alimalizia
hotuba yake DC huyo amewataka wananchi wote kushiriki zoezi la Sensa ya watu na
makazi itakayofanyika tarehe 23 Agost 2022.
Naye Mwenyekiti
wa Soko la vitunguu Misuna Iddy Swalehe Mwanja akatumia nafasi hiyo kuiomba
Wizara ya Kilimo pamoja na viwanda na Wizara ya viwanda na Biashara kusimamia
zoezi la upatikanaji wa vifungashio vya kutosha uwezo wa kubeba kilo Mia moja
kwa kuwa imeoneka kutopatika katika baadhi ya mikoa.
Amesema
Singida wapo tayari kutumia vifungashio vya neti ambavyo havimpunji mkulima
lakini ipo mikoa bado inaendelea kutumia rumbesa hivyo kusababisha wengine
kukosa soko la vitunguu.
Swalehe
ameendelea kuiomba Serikali kuyasimamia vizuizi vilivyopo barabarani kusimamia
kikamilifu ukaguzi wa rumbesa ili kusaidia kuondoa changamoto za ujazaji wa
bidhaa wa kupitiliza.
Mkutano huo
ulihudhuriwa na viongozi mbalimbali ya Serikalini pamoja na viongozi wa Soko na
Wananchi mbalimba walikuja kufanya usafi wa maeneo hayo.
Mwisho
No comments:
Post a Comment