Serikali za Vijiji Mkoani Singida zimetakiwa kutumia fursa za uwepo wa misitu inayowazunguka kwa kuitenga kama hifadhi ili kusaidia utunzaji wa mazingira na kuongeza kipatao kupitia utalii badala ya kutumika kwa ajili ya kuvuna mkaa ambao hauna faida.
Mkuu wa Mkoa Singida Dkt. Binilith Mahenge ametoa
kauli hiyo hivi karibu alipotembelea hifadhi ya mbuga za wanyama ya Rungwa
iliyopo wilayani Manyoni mkoani hapo na kubaini bado meneo hayo
hayajawanufaisha wanachi kwa kiwango kikubwa.
Amesema uwepo wa mapori na misitu katika maeneo ya vijiji ni fursa kubwa kama yataendeshwa ki mkakati ili yasaidi kufunga wanyama pori, kutunza mazingira na kuingizia kijiji mapato.
Dkt. Mahenge amebainisha kwamba vijiji vingi vimekuwa vikitumia misitu kwa ajili ya kuchoma mkaa na kusababisha uharibufu mkubwa wa mazingira ambapo kama misitu hiyo ingehifadhiwa wanyama wangekuwepo na utalii ungeshamiri jambo ambalo lingechangia kijiji kupata mapato makubwa.
Dkt. Mahenge akamtaka Mkurugenzi, Mwenyekiti wa
Halmashauri pamoja na DC wa Wilaya hiyo kuhakikisha kwamba misitu inatunzwa kwa
kushirikiana na Wakala wa hifadhi ya wanyamapori na vijiji kwa lengo la
kuwanufaisha wananchi.
“Ili kulinda mazingira vizuri na kuwaongezea wananchi mapato ni lazima kuanzisha mkakati wa kuhifadhi mazingira ki mkakati”
“Mkurugenzi, Mwenyekiti wa Halmashauri pamoja na Mkuu wa Wilaya nendeni mkakutane na wananchi wakapendekeze maeneo ambayo leo ni misitu ambayo wanavuna na wanachoma mkaa lakini hawapati faida. Alisistiza RC Mahenge.
Endapo maeneo hayo yatalindwa hakutakuwepo na migogoro, ujagili wala uingizaji wa mifugo na vijiji vitapata mapato. Alisistiza Dkt. Mahenge.
Kwa upande wake Muhifadhi Mkuu wa Mamlaka ya Wanyapori Tanzania (TAWA) Peter Malcery Erro akieleza mikakati iliyopo juu ya uhifadhi amesema aina ya utalii unafanyika katika hifadhi hiyo ni uwindaji katika vitalu ambapo mwenye kitalu analazimika kulipa milioni 130 kwa mwaka pamoja na asilimia 40 kwa wanyama aliowawinda bila kujali alipata au alikosa.
Tumejipanga kufanya uwekezaji mahiri ambao unagharimu dolla za kimarekani 10,000 kwa kutenga maeneo ya aina mbalimbali ili kuongeza kipato ikilinganishwa na sasa.
Muhifadhi Mkuu wa Mamlaka ya Wanyapori Tanzania (TAWA) Peter Malcery Erro akieleza mikakati iliyopo juu ya uhifadhi.
No comments:
Post a Comment