Mkuu wa Mkoa Singida Dkt.Binilithi Mahenge ametembelea mashamba makubwa yanayoandaliwa kwa ajili ya Kilimo cha alizeti wilayani Ikungi na kuzindua Msimu wa Kilimo kwa mwaka 2022 kwa wakulima wa kata ya Issuna wilayani hapo.
Akiwa katika mashamba hayo wameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi kwa kuanzisha kilimo cha mashamba makubwa cha pamoja (block farming) katika eneo lenye ukubwa wa Ekari 4800.
Amesema mashamba hayo makubwa ni maalum kwa ajili ya kilimo cha alizeti chenye lengo la kusaidia kupunguza tatizo la mafuta ya kula hapa nchini.
Ameitaka Halmashauri hiyo kuwasaidia wakulima upatikanaji wa matrekta kwa gharama nafuu yatakayo wasaidi kusafisha mashamba hayo.
RC Mahenge amebainisha kwamba Serikali tayari imeleta mbegu ya kutosheleza mahitaji ya wakulima waliojiandikisha kwa kilimo hicho ambapo zitagawiwa kwa wakulima hivi karibuni.
Aidha amesema Serikali ya Mkoa itakutana na Benki ya NMB kujadili namna ambayo wataweza kusaidia usafishaji na uendeshaji wa mashamba hayo ambayo tayari wakulima hao wamekwisha jiunga na ushirika.
Akizindua msimu wa kilimo amesema RC Mahenge amewataka vijana kujiunga katika vikundi ili waweze kukopesheka na kuongeza uzalishaji wa alizeti itakayotosheleza kulisha viwanda vya ndani.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe.Jerry Muro amemueleza mkuu wa Mkoa kwamba shamba hilo lina ukibwa wa Ekari 4500 zilizogawanywa Katika vipande vya Ekari 100.
DC Jerry ametoa wito wa wawekezaji kuwekeza katika ujenzi wa maghala kwa ajili ya kuhifadhia wakati wakulima wakisubiria soko na taratibu nyinginezo.
Aidha DC huyo amewataka vijana na akina mama kutumia fursa hiyo kushiriki katika kilimo, kuwekeza katika maduka ya pembejeo na pasitokee mtu kuzurula kwa kuwa utajiri umesogezwa mikononi mwao.
Hata hivyo Halmashauri ya Ikungi imedhamiria kuwasaidia wakulima hao wa alizeti katika mashamba makubwa kuwaunganisha na wenye zana za kilimo kwa ajili ya kusafisha maeneo hayo kwa gharama nafuu.
Katika hatua nyinge Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge walitembelea Skimu ya Umwagiliaji ya Mang'onyi iliyopo Kijiji cha Mwalu Kata ya Mang'onyi ili kusikiliza changamoto zinazowakabili wakulima wa skimu hiyo.
Skimu ya Mang'onyi inahudumia vijiji vitatu vya Tupendane, Mwau na Mang'onyi yenyewe ambapo ina ukibwa wa hekta 450 lakini zinazotumika ni hekta 50 ambazo ndio zeye miundombinu ya umwagiliaji.
Akiongea na wanakijiji wa maeneo hayo Dkt.Mahenge ameagiza mashamba pori yote katika eneo la skimu hiyo yasafishwe na kufanyiwa kazi zilizokusudiwa.
RC. Mahenge amesema kila mmiliki wa shamba katika skimu hiyo ahakikishe analiendeleza, vinginevyo yatagawiwa kwa wakulima wengine wenye uhitaji.
Hata hivyo ameagiza wakulima wote wanaofaidika na Skimu hiyo kuchangia mfuko wa Umwagiliaji ambao umekuwa ukitumika katika kukarabati miundombinu ya Skimu inapoharibika
Amesema Skimu hiyo ikitumika kwa ufanisi ina uwezo wa kulisha Mkoa mzima wa Singida na mikoa ya jirani.
Akimalizia hotuba yake Mkuu wa mkoa amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ikungi Bw. Justice Kijazi kutafuta fedha na kukarabati barabara inayoingia katika Skimu hiyo ili yawasaidie wakulima kusafirisha mazao yao kwa urahisi.
Wakiendelea na ziara katika Skimu hiyo DC. Jerry Muro akawataka wanufaika kuhakikisaha wachague viongozi ambao watasimamia na kuendeleza kilimo cha umwagiliaji kijijini hapo.
No comments:
Post a Comment