Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mheshimiwa Halima Dendego, ametoa shukrani zake za dhati kwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa juhudi kubwa za maendeleo zinazotekelezwa mkoani humo.
Akizungumza na wananchi katika Kata ya Iguguno Wilayani
Mkalama (Agosti 18, 2024) kwenye ziara ya Spika wa Baraza la Wawakilishi
Zanzibar Zubeir Ali Maulid, iliyolenga
kuhamasisha wananchi kushiriki kikamilifu Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024,
Dendego ameeleza kuwa Serikali chini ya Uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu
Hassan, imefanikisha utekelezaji wa
miradi mbalimbali inayogusa kila sekta, ikiwemo kilimo, miundombinu ya elimu,
maji, afya, uwekezaji, nishati ya umeme, barabara ambayo imeleta mafanikio makubwa
kwa wananchi wa Singida.
Akizungumza kuhusu sekta ya kilimo, Mheshimiwa Dendego amesema kuwa mkoa huo umefanikiwa kuzalisha chakula cha kutosha kutokana na uwekezaji mkubwa kwenye skimu za umwagiliaji.
"Licha ya changamoto ya mvua
kuwa ya kiasi, kupitia skimu hizi za umwagiliaji, tumefanikiwa kupata chakula
cha kutosha na tumefuta kabisa tabia ya kuomba msaada wa chakula," alisema
Dendego.
Mkoa wa Singida unajivunia kuwa na skimu za umwagiliaji
zipatazo 24 ambazo zimekuwa na mchango mkubwa katika uzalishaji wa mazao.
Aidha, Mkuu huyo wa mkoa
alibainisha kuwa wamefanikiwa kupata mbegu bora na ruzuku ya mbegu, hali
iliyowezesha kuzalisha zaidi ya tani tisa za chakula.
Kwa hatua hizi za maendeleo, RC Dendego amemshukuru sana Rais
Dkt. Samia kwa uongozi wake makini na uwekezaji mkubwa katika sekta ya kilimo
na nyinginezo, ambazo zimeleta tija kwa wakulima na wananchi wa Singida kwa
ujumla.
Hata hivyo, alisisitiza kuwa Serikali itaendelea kushirikiana
na wananchi kuhakikisha mkoa huo unazidi kupiga hatua kubwa zaidi katika
maendeleo.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Mheshimiwa Halima Dendego, akizungumza na wananchi wa Kata ya Iguguno Wilayani Mkalama kwenye ziara ya Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mheshimiwa Zubeir Ali Maulid iliyohusu kuhamasisha wananchi kushiriki kikamilifu Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27, 2024
No comments:
Post a Comment