Mkuu huyo wa
mkoa wa Singida ametoa agizo hilo (14 Agosti,
2024) katika majumuisho ya ziara yake ya kukagua miradi mbalimbali ya
Maendeleo katika Manispaa ya Singida.
Dendego
amesisitiza kuwa miradi yote iliyoanza kutekelezwa katika kipindi cha miaka
Mitatu nyuma lazima ikamilike ili wananchi waanze kupata huduma mbalimbali za
kijamii kwa muda muafaka.
“Lengo la miradi hii
sio kuona majengo bali ni kutoa huduma inayotakiwa lazima majengo yakamilike
kwa wakati na kwenye matatizo Viongozi wakae na kutatua changamoto hiyo ili
miradi isikwame, Ameeleza Dendego.
Ameeleza
kuwa maeneo yote ya miradi ambayo yana migogoro lazima Viongozi wakae wahusika
ili kuondoa changamoto hizo kwa wakati nia ikiwa ni kuona wananchi wanaanza kupata
huduma bora na za msingi karibu na maeneo yao.
Dendego pia
amepongeza hatua zinachukuliwa na Watendaji katika kusimamia na kutekeleza
miradi hiyo ya maendeleo ili iweze kutekelezwa kwa viwango na ubora unaotakiwa.
Kwa upande
wake, Katibu Tawala wa mkoa wa Singida Dkt. Fatuma Mganga amemhakikishia Mkuu
wa mkoa wa Singida kuwa atahakikisha miradi yote inayotekelezwa mkoani humo
inakamilika kwa wakati na kwa kuzingatia thamani ya fedha iliyotolewa.
Dkt. Mganga
amewasisitiza Watendaji wote washiriki kikamilifu katika kusimamia miradi
iliyopo kwenye maeneo yao ili wananchi waweze kufurahia huduma bora
zinazotolewa na Serikali yao.
Naye, Mkuu
wa Wilaya ya Singida Godwin Gondwe, ameeleza kuwa atafanya kazi kwa usiku na
mchana kwa ushirikiano na Watendaji wengine ili kuhakikisha miradi yote ya Maendeleo
inayotekelezwa kwenye Wilaya yake inakamilika hadi mwisho wa mwezi huu kama
maelekezo ya Serikali yanayotaka.
No comments:
Post a Comment