Akizindua zoezi la utoaji wa Chanjo hiyo katika Kijiji cha Kisaki
Manispaa ya Singida, Mkuu wa mkoa wa Singida Mheshimiwa Halima Dendego (leo 22-Aprili-2024 ) amewaagiza
Maafisa Afya wahakikishe maeneo yote yaliyoandaliwa kutolewa huduma hiyo ya
chanjo yanafanya hivyo kwa viwango vya juu ili kuwalinda watoto wa kike na
saratani hiyo hatari.
Dendego amesisitiza kuwa chanjo hiyo pia ni lazima iwafikie
wanafunzi wanaosoma kwenye shule binafsi na watoto wa kike ambao wanaishi mitaani
nao wapate fursa ya kupata chanjo hiyo ili kuwakinga na saratari na mlango wa kizazi.
“Tunapoenda
kuwalinda watoto wa kike kwa kuwachanja chanjo hiyo maana yake tunawaepusha na
madhara ugonjwa wa saratani ili wasije wakaambukiza wavulana”Ameeleza RC. Halima
Dendego.
Amesisitiza kuwa chanjo hiyo ni muhimu kwa wasichana na inatolewa
bure kwa sababu Serikali kwa kushirikiana na Wadau wa maendeleo imegharamia
chanjo hiyo, hivyo ni muhimu kwa wazazi na walezi kuwapeleka watoto wao kupata
chanjo hiyo ili kuwaepusha na madhara yanayoweza kutokea.
Kwaupande wake, Mganga Mkuu mkoa wa Singida Dkt. Victorina
Ludovick amesema kwa Tanzania chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi (HPV)
ilianza majaribio mwaka 2014 mkoani Kilimanjaro na kupata mafanikio makubwa kwa
kuwakinga wasichana wasipate ugonjwa huo.
Dkt. Victorina Ludovick ameeleza mtu yeyote anaweza kuambukizwa
saratani hiyo katika umri wowote ule hasa wakati wa tendo la ndoa na inaweza
kusababisha magonjwa mengine ikiwemo saratani ya koo na magonjwa mengine ya via
vya kizazi kwa wanamke na wanaume.
Naye, Katibu Tawala wa mkoa wa Singida Dkt. Fatuma Mganga
amewataka Maafisa Afya wanaotoa chanjo hiyo kuhakikisha wanafanikisha zoezi
hilo kwa viwango ili mkoa wa Singida uwe wa kwanza katika utoaji wa chanjo hiyo
kwa wasichana mwenye umri wa miaka Tisa hadi 14.
Amesema saratani hiyo inaua na ni ugonjwa hatari hivyo ni muhimu
kwa watoto wote wenye umri wa kupata chanjo wapewe kutokana na umuhimu wake
katika kulinda afya zao.
Nao, Mashuhuda waliopewa chanjo hiyo wakizungumza kwenye uzinduzi
wa utoaji wa chanjo ya satarani la mlango wa kizazi katika kijiji cha Kisaki
Manispaa ya Singida Lukuresia Andrea na Salisabila Athumani wote wakazi wa mkoa
wa Singida wamesema tangu wapatiwe chanjo hiyo hawajapata madhara yoyote hivyo
wameomba wazazi na walezi wasiwazuie watoto wao wa kike kwenda kupata chanjo
hiyo kwa sababu inafaida kubwa katika maisha yao.
Zoezi la kuimarisha chanjo ya HPV litakamilika tarehe 26 Aprili,
2024 hata hivyo hudumaa hiyo itaendelea kutolewa kwa utaratibu wa zamani yaani
shuleni, vituo vya kutolea huduma za afya na kwenye huduma za mkoba za Masuala
ya Afya ya Uzazi na Mtoto.
Chanjo ya HPV, kama ilivyo kwa chanjo nyingine zinazotolewa
kupitia Mpango wa Taifa wa Chanjo, haiuzwi kwa mteja yeyote, hivyo inatolewa
bure kwa walengwa katika vituo vyetu vya kutolea huduma.
Baadhi ya Wanawake waliopata chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi mkoani Singida wakiwa na watoto wao.
No comments:
Post a Comment