Wednesday, August 16, 2023

SINGIDA YAJA NA MKAKATI MPYA WA KUPANDISHA KIWANGO CHA UFAULU KWA SHULE ...


Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba ameziagiza Halmashauri za Mkoa huo kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili Walimu wa shule za Msingi na Sekondari ili kuwawezesha kutekeleza majukumu yao ipasavyo sambamba na kuongeza hali ya ufaulu kwa wanafunzi.

Serukamba ametoa maagizo hayo jana (tarehe 15 Agosti, 2023) katika mkutano maalumu uliofanyika katika ukumbi wa mikutano Social uliyopo Singida Mjini, uliyokutanisha wadau mbalimbali wa sekta ya elimu mkoani hapo kwa lengo la kuboresha hali ya taalum.

Aidha, Mkuu huyo wa Mkoa amesema, amewapongeza watendaji kwa kujenga na kusimamia kwa kiwango kikubwa utekelezaji wa  miradi ya ujenzi kwa kukamilisha kwa wakati na ubora miundombinu ya elimu isipokuwa hakuridhishwa na hali ya ufauli wa wanafunzi wa darasa la saba na kidato cha nne.


No comments:

Post a Comment