Wednesday, April 26, 2023

Singida wapongezwa kusherehekea Muungano kwa kushiriki ujenzi

Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba amewapongeza wananchi wa Mkoa huo kwa kujitokeza kufanya kazi za mikono katika Ujenzi wa shule ya msingi Minga iliyopo Manispaa ya Singida ambapo wameweza kuchimba msingi katika vyumba 16 vya madarasa na shimo la choo pamoja na upandaji miti.

Akiongea katika hotuba baada ya kumaliza kazi, RC Serukamba amesema kazi hiyo imeleta tija kubwa kwa kuwa itasaidia wanafunzi zaidi ya 889 kupata sehemu za kusomea.

RC amesema jumla ya vyumba 16 vitajengwa kupitia mradi wa boost ambapo kila darasa amesema litagharimu shilingi Milioni 23 ambapo shule ya awali itagharimu Milioni 63.6

Aidha ameeleza kwamba majengo mengine ni jengo la utawala litakalogharimu Milioni 71.5 kichomea taka shilingi Milioni 5.7 matundu ya vyoo 18 yatakayo gharimu Milioni 1.7 fedha ambazo zimetoka kwenye Mradi wa Boost.

Akiwa katika uadhimishaji wa maadhisho hayo Serukamba ameagiza taasisi watu binafsi na mashirika kuhakikisha wanapanda miti na kufanya usafi kila sehemu huku akiwataka wananchi kutoa kodi za taka ili kusaidia maeneo yao kuwa safi.

Kwa upande wake Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dkt. Fatma Mganga amesema Wilaya zote za Mkoa huo zimejumuika katika kushiriki ujenzi wa shule hiyo baada ya kufanya usafi na kupanda miti katika Wilaya zao hapo jana na juzi.

Amesema miradi hiyo ya shule imegawanywa katika wilaya ambapo zipo zilizopata shule mbili na nyingine shule moja kulingana na mahitaji huku akiwakumbusha Wakurugenzi kuendelea kuchongesha madawati ili yatakapokamilika yaweze kutumika kwa wakati.

Hata hivyo amezishukuru taasisi mbalimbali kwa namna mbalimbali ambavyo walivyosherehekea Muungano ikiwemo kupamba Ofisi zao na kufanya usafi maeneo yanayowazunguka.

Ameyashukru makampuni na taasisi za fedha ikiwemo NMB kwa kutoa mchango wao mkubwa wa vihifazia taka kwa lengo la kudumisha usafi.

MATUKIO MBALIMBALI KATIKA PICHA






















No comments:

Post a Comment