Maelezo hayo ameyatoa leo katika ukumbi wa mikutano wa
Halmashauri hiyo alipokuwa akitatua kero za Wananchi waliokuwa wakilalamikia
uwepo wa mbuzi wanaozurura mitaani na kuharibu miti na mazao mengine
yaliyopandwa.
Akitolea ufafanuzi swala hilo Mkuu wa Mkoa huyo amemuagiza aliyekuwa akikaimu nafafasi ya Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Huseni Sepoko kuhakikisha kwamba katika kipindi kifupi wawe wametunga Sheria ndogo ambazo zitawasaidia kuzuia wanyama wanaorandaranda ambayo itaruhusu kuwakamata mifugo hiyo na kuwapiga faini.
"Nakuagiza Mkurugenzi katika kipindi kifupi kijacho
mtunge Sheria ndogo ambazo zitazuia mifugo kuzurura mitaani, na mhakikishe Sheria
hiyo inaweza kutoa adhabu kali kwa watakao kiuka utaratibu". RC Serukamba
Amesema kwa sasa ni mpango wa Mkoa kuhakikisha kwamba kunapandwa
miti zaidi ya Milioni tatu na kuifanya Singida kuwa mji wa kijani jambo ambalo
haliwezi kufanikiwa endapo miti hiyo itaendelea kuharibiwa na mbuzi wazururao.
"Mkoa tumepanga kupanda miti zaidi ya Milioni tatu,
tutashirikiana na wanafunzi, Makanisa na Misikiti kuhakikisha kila kaya inakuwa
na miti isiyopungua minne, hatutavumilia jitihada hizo zikwamishwe kwa
uzembe" Serukamba.
Aidha amewataka viongozi wa Halmashauri hiyo kuhakikisha wanawafuata wananchi walipo na kutatua kero zao badala ya kukaa ofsini kusubiri viongozi wa ngazi ya juu wanapotoka na kila mtumishi ahakikishe anakamilisha majukumu yake kwa wakati.
Akiwa katika ziara hiyo Mkuu wa Mkoa ameweza kusikiliza jumla ya kero 32 zikiwemo za ardhi, maji na madeni na usafi wa Mazingira.
No comments:
Post a Comment