Wednesday, August 24, 2022

Serikali yatoa power benk 200 Mkoani Singida kwa ajili ya vishkwambi vya Makarani wa Sensa.

 

Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba (kushoto) akizungumza na Karani wa Sensa (mwenye kishikwambi) wakati wa ziara wilayani Singida vijijini.

Serikali imetoa power benk 200 katika maeneo ambayo yanachangamoto ya ukosefu wa umeme Mkoani Singida kama sehemu ya utatuzi wa changamoto ya kuishiwa chaji kwa vishikwambi ambavyo vinatumiwa na Makarani wa Sensa ya watu na Makazi ya 2022.

Akiongea baada ya kuwatembelea Makarani hao katika Manispaa ya Singida, Singida Dc na Wilaya ya Mkalama Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba amesema Serikali imetoa Power Benk hizo kwa kuwa jana uzoefu umeonesha baadhi ya maeneo Makarani kupata changamoto baada ya vitendea kazi vyao kumaliza chaji kabla ya muda.

Amesema kutokana na ukaguzi alioufanya kupitia Makarani wapata Tisa ameona zoezi linaendelea vizuri na kuna kila dalili ya kumaliza zoezi hilo ndani ya muda na kila mwananchi kufikiwa.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba (wa tatu kutoka kushoto) akizungumza na Karani wa Sensa wakati wa ziara wilayani Singida vijijini.

RC Serukamba amawaomba wananchi wa Mkoa huo kutoa ushirikiano mkubwa kwa Makarani ikiwemo kuwaruhusu kuchaji vishikwambi vyao kwenye makazi yao wakati wakiendelea kuhesabu.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhandisi Paskas Muragili amesema zoezi linaendela vizuri na haijatokea changamoto yoyote kwa kuwa wataalamu wa tehema wamekuwa karibu na Makarani kwa ajili ya utatuzi wa changamoto yoyote itakayojitokeza.

Aidha amemhakikishia Mkuu wa Mkoa kwamba kwa upande wa Wilaya ya Singida wanategemea mafanikio makubwa kama walivyotegemea.

Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Sophia Kizigo akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya ziara ya Mkuu wa Mkoa huo kujionea maendeleo ya zoezi la Sensa katika mkoa wa Singida.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Sophia Kizigo ameeleza kwamba changamoto ya kuishiwa chaji imejitokeza kwa Makarani wa Wilaya hiyo kwenye vijiji ambavyo havijapata huduma ya umeme.

Hata hivyo amemuomba Mkuu wa Mkoa katika Power benk zilizokuja Wilaya hiyo ipewe kipaumbele kwa kuwa pamoja na changamoto ya umeme kwa ajili ya kuchaji lakini bado kuna umbali wa nyumba hadi nyumba.

Kizigo amewataka wananchi ambao bado hawajahesabiwa kuhakikisha kuendelea kuwa na subira kwa kukuwa katika kipindi cha siku Tano zilizobaki watahakikisha kila mwananchi anafikiwa.

Aidha Mratibu wa Sensa Mkoa wa Singida Naing'oya Kipuyo amekiri kupokea power benk hizo ambazo zitakuwa msaada mkubwa kwa Makarani waliyopangiwa Vijijini ambapo hakuna Umeme.

MATUKIO MBALIMBALI WAKATI WA ZIARA YA RC SERUKAMBA 

Mratibu wa Sensa Mkoa wa Singida Naing'oya Kipuyo akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya ziara ya Mkuu wa Mkoa kukamilika.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba akisikiliza jambo kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhandisi Paskas Muragili ( wa pili kutoka kushoto) na Mratibu wa Sensa Mkoa wa Singida Naing'oya Kipuyo wakati wa ziara wilayani Singida vijijini.




Mkuu wa Mkoa wa Singida akizungumza na Makarani wa Sensa wakati wa ziara yake.



Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba (wapili kutoka kushoto) akiongozo jopo la viongozi na waratibu wa Sensa Mkoa na ngazi ya Halmashauri za mkoa huo kuelekea kwenye moja ya Kaya ambapo zoezi la Sensa linaendelea ili kujionea hali halisi ya utekelezaji wa zoezi hilo.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba akisisitiza jambo wakati wa ziara yake.

RC Serukamba akizungumza na Waandishi wa habari mara baara ya kukamilisha ziara yake ya kujionea maendeleo ya zoezi la Sensa ya Watu na Makazi linaloendelea mkoani Singida leo Agosti 24, 2022.

No comments:

Post a Comment