Tuesday, August 09, 2022

Mwenge wa Uhuru Wazindua Miradi miwili, miwili yakaguliwa na miwili yatembelewa yenye thamani ya Tsh. Bilioni 1.8 Wilayani Iramba

Mwenge wa Uhuru Wilayani Iramba umekamilisha ziara yake kwa kukagua, kuweka jiwe la msingi na kuzindua miradi 6 ikiwa ni pamoja kutembelea vikundi vya wajasiriamali.

Katika taarifa yake Mkuu wa Wilaya hiyo Suleiman Mwenda alisema Mwenge umekimbizwa kwa umbali wa km 127.7 ambapo miradi miwili ilitembelewa, miwili kukaguliwa na miwili kuzinduliwa.

Mwenda amebainisha kwamba miradi hiyo imegharimu kiasi cha Tsh. Bilioni 1.8 ambapo baadhi ya miradi imehusisha michango ya wananchi.

Miradi hiyo ilikuwa Barabara ya Shelui Nkyala yenye urefu wa Km 5, nyumba ya Watumishi wa Kituo cha Afya, Ujenzi wa shule ya Sekondari, jengo la dharura na jengo la wangonjwa mahututi.

Aidha klabu za kupinga matumizi ya madawa ya kulevya, kupinga rushwa na vikundi vya wajasiriamali vilitembelewa.

Kwa upande wake Sahili Nyanzabara Geraruma Kiongozi wa Mbio za Mwenge aliwataka Wahandisi kufanyia kazi changamoto ndogo ndogo zilizojitokeza katika miradi ya Barabara na baadhi katika majengo hayo.

Amewataka wazazi na walimu kushirikiana kuhakikisha kwamba watoto hawashiriki vitendo vya uvunjifu wa amani na kuhakikisha wanakomesha rushwa na matumizi ya madawa ya kulevya.

Hata hivyo Kiongozi huyo akitoa ujumbe wa Sensa ya Watu na Makazi amewataka wananchi kujitokeza kuhesabiwa tarehe 23.08.2022

Hata hivyo Mwenge utaendelea na ukaguzi wa miradi mbalimbali ya Maendeleo katika Wilaya ya Mkalama.

No comments:

Post a Comment