Wednesday, August 10, 2022

Mwenge wa Uhuru umepokelewa Wilayani Mkalama ambapo utakimbizwa Kilometa 129 na kukagua Miradi Mitano na Programu Tano.

 

Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Sophia Kizigo akiwa ameubeba Mwenge wa Uhuru wakati wa mapokezi ya Mbio za Mwenge wa Uhuru wilayani humo Agosti 10, 2022

Akiongea wakati wa makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru huo kutoka Wilaya ya Iramba, Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Sophia Kizigo amesema kwamba Mwenge utakagua miradi ya Ujenzi wa shule kupitia fedha za Uviko Vituo vya Afya na Miradi ya Lishe.

DC Kizigo amebainisha kwamba mbio hizo za Mwenge wa Uhuru zitakagua miradi hiyo ambayo imegharimu jumla ya Tsh. Bilioni 1.34 na kwamba utawasaidia wananchi wengi wa Wilaya hiyo.

Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Sophia Kizigo akizungumza na Wananchi wakati wa mapokezi ya Mbio za Mwenge wa Uhuru wilayani humo Agosti 10, 2022

Aidha DC Kizigo amesema kwamba miradi hiyo ni muhimu sana kwenye maisha ya watu wakiwemo wanafunzi ambapo katika programu ya Lishe wameweza kuzalisha mboga zenye virutubishi vingi na muhimu kwa Afya.

Awali akikabidhi Mwenge wa Uhuru, DC Suleiman Mwenda aliwakumbusha wana Mkalama kujipanga vizuri ikiwa ni pamoja na kuandaa nyaraka halisi za miradi hiyo.

Kwa upande wake Kiongozi wa Mbio za Mwenge  Sahili Nyanzabara Gerurama  ameanza kwa kutoa neno la Sensa ambapo amewataka wananchi kujitokeza kuhesabiwa  tarehe 23.8.2022 katika kukamilisha zoezi la Sensa ya watu na makazi.

Aidha amewataka viongozi katika Halmashauri hiyo pamoja na Wahandisi husika kuhakikisha katika eneo la Mradi kunakuwepo na nyaraka zinazotakiwa na watu watakaoweza kutoa maelezo sahihi.

Mwisho

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama Asia Juma Messos akiwa ameubeba Mwenge wa Uhuru wakati wa mapokezi ya Mbio za Mwenge wa Uhuru wilayani humo Agosti 10, 2022

Mapokezi ya Mbio za Mwenge wa Uhuru yakiendelea wilayani humo Agosti 10, 2022


No comments:

Post a Comment