Thursday, July 14, 2022

ZIARA YA WAZIRI MKUU MKOANI SINGIDA KUANZIA TAREHE 15-19/07/2022

WAZIRI Mkuu, Kassimu Majaliwa, anatarajia kufanya ziara ya siku nne mkoani Singida ambapo pamoja na mambo mengine atakagua miradi ya maendeleo na kuweka jiwe la msingi katika miradi mbalimbali.

Kwamujibu wa ratiba iliyotolewa na ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida, imeeleza kuwa Waziri Mkuu atanza ziara hiyo kesho Julai 15 hadi Juali 19, 2022 ambapo ataanzia katika Wilaya ya Manyoni.

Akiwa katika kata ya Solya Wilaya ya Manyoni, atapokea taarifa ya ujenzi wa Sekondari ya Wasichana Solya na kuweka jiwe la msingi na baadaye kupokea taarifa ya mkoa na kisha kuzungumza na watumishi.

Aidha,Waziri Mkuu atapokea taarifa na kutembelea ujenzi wa barabara ya kilometa 10 Itigi mjini na baadaye kuzungumza na wananchi na jioni ataweka jiwe la msingi mradi wa ujenzi wa kituo cha afya Mtoa na kisha kuzungumza na wananchi.

Julai 16, Waziri Mkuu, atawasili Wilayani Iramba ambapo atatembelea mradi wa maji Misigiri,atazungumza na wananchi  pamoja na  watumishi.

Aidha, Waziri Mkuu, Majaliwa atakuwa katika Wilaya ya Makalama ambako atatembelea mradi wa ujenzi wa daraja la mawe na baadaye mchana atazindua ofisi ya Mkuu wa Wilaya Mkalama na kusalimiana na wananchi.

Julai 18, atakuwa katika Wilaya ya Ikungi, atapokea taarifa na kutembelea mradi wa ujenzi wa kituo cha afya Irisya na mchana atatembelea makazi ya viongozi wa kitaifa.

Baadaye ataweka jiwe la msingi ujenzi wa Chuo cha VETA na Hospitali ya Wilaya na kisha kuongea na wananchi.

Waziri Mkuu atahitimisha ziara yake katika Wilaya ya Singida Julai 19, kwa kuweka jiwe la msingi ujenzi wa ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Singida na kuzungumza na wananchi.

Baadaye Waziri Mkuu, atatembelea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida na kuzungumza na watumishi.

MWISHO

No comments:

Post a Comment