Mkuu wa Mkoa
wa Singida Dkt. Binilith Mahenge amewataka wasimamizi wa mradi wa kilimo cha
korosho cha pamoja kufunga akaunti zote za benki pamoja na kusimamisha upokeaji
wa fedha kwa ajili ya ugawaji na usafishaji wa mashamba hayo mpaka
watakapokamilisha zoezi la uhakiki kwa kulinganisha na fedha walizopokea na
idadi ya mashamba.
Akiongea
wakati wa kikao kilichohusisha kamati ya wilaya ya ulinzi na usalama, viongozi
mbalimbali wa mkoa na wasimamizi wa
mradi wa mashamba ya korosho kilichofanyika hivi karibuni katika ukumbi
wa Halmashauri ya wilaya ya Manyoni, Dkt. Mahenge amesema mradi huo umekuwa
ukilalamikiwa na wadau wengi kwamba wamekuwa wakilipia fedha lakini hawajaoneshwa mashamba yao huku
wengine wakidai kubadilishiwa mashamba na kutosafishiwa kama walivyolipia fedha
zao.
Amesema
tathimini hiyo iwasaidie kubaini kiasi cha fedha walizopokea na ukubwa wa
mashamba waliyonayo ili busara zitumike kwa kufanya mawasiliano na wilaya za
jirani ili kuweza kugawa mashamba mengine au kurudisha fedha.
Aidha RC. Mahenge
akawataka viongozi hao kuandaa na kumkabidhi
taarifa ya kuanzia mwaka 2017 itakayoonesha kiasi cha mashamba
yaliyopimwa fedha zilizoingia na namna zilivyotumika kwa kila mwaka pamoja na
changamoto zilizojitokeza ndani ya siku zisizozidi siku saba.
Hata hivyo
amewataka viongozi wa mradi huo kuhakikisha unakamilika na unatoa huduma kwa
wananchi kama ilivyokuwa imepangwa
No comments:
Post a Comment