Friday, September 24, 2021

WATAALAM WALIOPATA MAFUNZO YA CHANJO YA UVIKO 19 WATAKIWA KUPELEKA ELIMU KWA JAMII

 

Mganga Mkuu Mkoa wa Singida, Victorin Ludovick akisisitiza jambo wakati wa mafunzo. 

Mafunzo ya wataalamu wa afya  na viongozi mbalimbali wametakiwa kusambaza elimu ya chanjo ya UVIKO 19 katika vituo mbalimbali vinavyotoa chanjo  na kwenye mikusanyiko ya watu ili kusaidia kupunguza athari  za ugonjwa huo.

Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya Siku mbili yaliyofanyika mkoani Singida na kuwahusisha Waganga wakuu wa Wilaya,  Maafisa habari  na baadhi ya wawakilishi kutoka wizara mbalimbali, Mganga Mkuu wa Mkoa, Victorin Ludovick amesema  kumalizika kwa mafunzo hayo ndio mwanzo wa kutoa elimu kwa watoa chanjo na wananchi kwa ujumla.

Amesema elimu waliyopata wakufunzi hao wataenda kuwafundisha wengine kuanzia ngazi ya Halmashauri mpaka Vijijini

Dkt.Ludovick amesema elimu  waliyopata imetoa muongozo wa  utoaji wa elimu  sehemu mbalimbali ikiwemo minadani na kwenye masoko na sehemu zenye watu wengi.

Mafunzo yamefanya zoezi la utoaji wa elimu ya chanjo  kuwa jepesi kwakuwa wataalamu wengi walishapata uzoefu mkubwa kwenye mambo ya utoaji wa chanzo. Alisema Mganga Mkuu wa Serikali.

"Mazoezi kama haya tushayafanya sana kwa hiyo naamini tunaenda kutekeleza tulichojifunza na nategemea kuona matokeo makubwa" alisistiza Dkt. Ludovick.

Pamoja na mafunzo hayo Dkt Victorine amesema mafunzo hayo yatumike  kubuni njia mbadala ya kuwafikia wananchi ili kuwaelimisha na kuhamasisha chanjo kwa kila mtu.

Amebainisha kwamba njia nyingine ni kuwatumia  viongozi wa dini ili wafikishe ujumbe kwa waumini wao juu ya umujimu wa kupata chanjo na kuondoa imani potofu kwa jamii dhidi ya chanjo ya UVIKO 19

Awali Mwakilishi wa Ofisi ya Rais -  TAMISEMI, Dinah Atinda  amesisitiza kuwa mafunzo hayo yanalenga kuwajengea uwezo watoa huduma za afya na pia viongozi na watu maarufu katika jamii husika ili waweze kuelimisha na kuhamasisha wananchi juu ya UVIKO-19 .

Amesema Mpango Jamii Shirikishi na Harakishi wa Chanjo dhidi ya UVIKO-19 umeandaliwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto  kwa kushirikiana na OR - TAMISEMI  na unaendelea kutekelezwa nchi nzima.

Hata hivyo amebainisha lengo la mafunzo hayo kuwa ni  kuwajengea uwezo watoa huduma za afya , viongozi na watu maarufu katika jamii husika ili  kuelimisha na kuhamasisha wananchi kuendelea kuchukua tahadhari ya ugonjwa wa UVIKO-19 na kupata chanjo dhidi ya ugonjwa huu.

Matukio mbalimbali katika picha

Mganga Mkuu Mkoa wa Singida, Victorin Ludovick akisisitiza jambo wakati wa mafunzo. (Katika) Mwakilishi wa Ofisi ya Rais -  TAMISEMI, Dinah Atinda na (kulia) Mshauri wa Ugavi kutoka shirika la JSI wanaoshirikiana na Wizara ya Afya kupitia Idara ya chanjo.  

Mwakilishi wa Ofisi ya Rais -  TAMISEMI, Dinah Atinda  akisisitiza jambo wakati wa mafunzo

Mafunzo yakiendelea, kulia ni Mganga Mkuu wa Mkoa Singida Victorin Ludovick

Afisa Mpango wa Chanjo kutoka Wizara ya Afya - TAMISEMI, Mpango wa Taifa wa chanjo Richard Magodi (kushoto) akizungumza wakati wa mafunzo hayo. 

Mganga Mkuu Halmashauri ya Wilaya ya Itigi ambaye pia aliyekuwa mwenyekiti wa Waganga wa halmashauri za mkoa wa Singida, Emmanuel Mallage akiishukuru Serikali kwa kuandaa mafunzo hayo kwa watoa huduma za afya katika ngazi zote za mkoa wa Singida.

Washiriki wa mafunzo hayo wakipongeza jambo

Picha ya pamoja na timu ya uendeshaji na usimamizi wa huduma za afya katika halmashauri ya Wilaya ya Itigi mkoani Singida

Picha ya pamoja na timu ya uendeshaji na usimamizi wa huduma za afya katika halmashauri ya Wilaya ya Iramba mkoani Singida

Picha ya pamoja na timu ya uendeshaji na usimamizi wa huduma za afya katika halmashauri ya Wilaya ya Mkalama mkoani Singida


Picha ya pamoja na timu ya uendeshaji na usimamizi wa huduma za afya katika halmashauri ya Manispaa ya Singida


Viongozi mbalimbali wa Serikali na Maafisa Watendaji (walio kaa) wakiwa katika picha ya pamoja na timu ya uendeshaji na usimamizi wa huduma za afya mkoa wa Singida muda mfupi baada ya kumaliza mafunzo kuhusu Mpango Shirikishi na Harakishi wa Chanjo ya UVIKO 19 kwa wakufunzi na wadau wa afya mkoani Singida. Septemba 23 - 24/2021 

No comments:

Post a Comment