Thursday, October 31, 2019

WANANCHI MKOANI SINGIDA WATAKIWA KUJIEPUSHA NA MAJANGA YA MOTO YATOKANAYO NA UZEMBE

MKUU wa mkoa wa Singida, Dkt Rehema Nchimbi amewataka wananchi kujiepusha na majanga ya moto yanayotokana na uzembe au makusudi kwa kigezo cha kutegemea uwepo wa Jeshi la Zimamoto
Dkt. Nchimbi aliyasema hayo Oktoba 31, 2019 wakati akikabidhi gari aina ya ‘Land Lover Defender’ kwa Jeshi la Zimamoto mkoani hapa litakalotumika kwa shughuli mbalimbali za utawala.
“Natarajia gari hili litasaidia kurahisisha majukumu ya kijeshi kwa Jeshi hili, hususan kwenye eneo la utoaji elimu na kujenga maarifa kwa jamii katika kuhakikisha suala la kinga linapewa kipaumbele ili kuepusha maafa na ajali zozote huko mbeleni,” alisema Nchimbi
Kwa upande wake, Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACF) Ivo Ombella, Kamanda wa Jeshi hilo mkoani hapa, alisema gari hilo litatumika kwa shughuli zote za dharula ndani ya jeshi hili chini ya uratibu wa idara ya utawala.
“Ifahamike kuwa Jeshi la Zimamoto linahusika na dharula zote ikiwemo majanga ya moto, tetemeko la ardhi, mafuriko na uzazi isipokuwa jinai pekee,” alisema Ombella
Aidha, aliwatahadharisha wananchi kuwa makini kwa kujiepusha na majanga ya moto hasa nyakati za utayarishaji wa mashamba kwa kuzingatia usalama na utunzaji mzuri wa mazingira kulingana na eneo husika.

MATUKIO KATIKA PICHA


Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Singida ikilitazama gari aina ya ‘Land Lover Defender’ kabla ya kulikabidhi kwa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoani hapa litakalotumika kwa shughuli mbalimbali za utawala.

Gari aina ya ‘Land Lover Defender’ lililokabidhiwa kwa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Singida litakalotumika kwa shughuli mbalimbali za utawala.

Mkuu wa Mkoa wa Singida akizungumza wakati wa kulikabidhi gari kwa Jeshi la Zimamoto  na Uokoaji mkoani hapa litakalotumika kwa shughuli mbalimbali za utawala.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akimkabidhi ufunguo wa gari aina ya ‘Land Lover Defender’ kwa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Singida litakalotumika kwa shughuli mbalimbali za utawala.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akipeana wakipeana mikono na Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACF) Ivo Ombella, Kamanda wa Jeshi hilo mkoa wa Singida  mara baada ya makabidhiano ya gari aina ya ‘Land Lover Defender’ kwa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Singida litakalotumika kwa shughuli mbalimbali za utawala.

Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACF) Ivo Ombella, Kamanda wa Jeshi hilo mkoa wa Singida akizungumza mara baada ya kukabidhiwa gari.

Picha ya pamoja kwa baadhi ya Jeshi la ZIMAMOTO na na Uokoaji mkoa wa Singida

Habari zaidi tembelea tovuti  http://www.singida.go.tz/

No comments:

Post a Comment