Fisi aliyezua tafrani Mjini Singida akiwa amejificha kutokana na kukimbizwa na wakazi wa mjini Singida.
Katika hali isiyo ya
kawaida wakazi wa manispaa ya Singida wameingiwa na taharuki na kuanza kukimbia
ovyo baada fisi kuonekakana katikati ya mji wa Singida akiwa anakimbia na
kuingia katika maduka ya wafanya biashara.
Wakieleza kwa hisia
tofauti baadhi ya wakazi huku wengine wakiwa wamepanda juu ya mapaa ya nyumba
pamoja na watoto wao kwa hofu ya kuumwa,wamesema kuonekana kwa fisi mjini
katikati ni jambo la ajabu kwani wanyama kama hao huonekana vijijini au porini,
wengine wamesema labda myama huyo amechelewa kurudi vichakani wakati alipokuwa
amekuja kula mabaki ya chakula mjini.
Baadhi
ya wakazi wa mji wa Singida wakitamaza askari polisi wakimchukua fisi aliyezua
tafrani Singida.
Akielezea tukio hilo
afisa maliasili mkoa wa Singida Bwana Charles Kidua amesema pamoja na kwamba
wanyama kama fisi wapo katika manispaa ya Singida na pindi wanapo onekana
katika maeneo ambayo siyo ya kawaida, wananchi watoe taarifa kwa mamlaka husika
kwani wanyama kama hao wanaweza kuwa na ugonjwa wa kichaa, badala ya
kujichukulia hatua mkononi ya kuwauwa.
Kutokana na umati wa
wananchi kuwa wengi wakati wakimfukuza fisi huyo bila kujali askari waliokuwa
wakituliza fujo huku wakiwa na silaha,wananchi walifanikiwa kuwapokonya askari
fisi baada ya kumtega na kamba huku wakiimba tunataka fisi wetu na kuamua
kumkimbiza mjini huku wakimpiga umbali wa kilomita mbili.
Baadhi
ya askari polisi wakihakikisha ulinzi na usalama unakuwepo wakati wa tafrani ya kumkamata fisi mjini Singida.
Fisi alizua tafrani akiwa ameuawa na kuweka katika gari la polisi mjini Singida.
Taarifa na picha kwa hisani ya blog ya Mpekuzihuru.
No comments:
Post a Comment