Mwenyekiti wa Bodi ya barabara ya Mkoa wa Singida, Mkuu wa Mkoa wa
Singida Dkt. Parseko V. Kone (katikati) akiendesha kikao cha 36 cha Bodi
ya barabara ya Mkoa wa Singida leo asubuhi, Kulia kwake ni Makamu
Mwenyekiti wa Bodi ya barabara ya Mkoa wa Singida, Mbunge wa Singida
Magharibi Mohamedi Misanga, na kulia kwake ni Katibu wa Bodi hiyo Katibu
Tawala Mkoa wa Singida, Liana Hassan.
Mkuu wa Mkoa wa Singida
Dkt. Parseko. V. Kone amewataka watendaji wote wa Mkoa wa Singida kuwahudumia
wananchi kwa wakati bila ya kusubiri vikao kwani kwa kufanya hivyo ni
kuchelewesha huduma kwa Wananchi.
Dkt. Kone ameyasema hayo
leo asubuhi katika kikao cha 36 cha bodi ya barabara ya Mkoa wa Singida huku
akisisitiza kuwa kufanya hivyo ni kutaka kuonekana kwenye vyombo vya habari huku
huduma kwa wananchi zikicheleweshwa.
Aidha amesema sekta ya
barabara ni miongoni mwa sekta ambazo zimeainishwa na Serikali katika Mpango wa
Matokeo Makubwa sasa hivyo usimamizi na utunzaji wa barabara utaharakisha
ukuaji wa uchumi wa wananchi.
Dkt Kone amesema sekta
ya barabara inaigharimu Serikali fedha nyingi, hivyo ni lazima kuhakikisha kuwa
thamani ya fedha zinazotolewa na Serikali au wafadhili zinalingana na uhalisia
wa matumizi yaliokusudiwa.
Pia amewataka watendaji
kuwashirikisha wananchi katika mipango, utekelezaji, usimamizi na tathmini za miradi
ya barabara kwani wananchi hao wanaweze kuwa walinzi wa barabara hizo ili zidumu
na zitumike kwa malengo yaliyokusudiwa.
Wajumbe wa Bodi ya Barabara, wa kwanza ni Mkuu wa Wilaya ya Singida Queen Mlozi, akifuatiwa na Mkuu wa Wilaya ya Iramba Yahaya Nawanda na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Manju Msambya wakifuatilia kikao hicho.
Wajumbe wa Bodi ya Barabara, wa kwanza ni Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Fatma Toufiq akifuatiwa na Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Edward Ole Lenga wakifuatilia kikao hicho.
Pia amewataka watendaji
kuwashirikisha wananchi katika mipango, utekelezaji, usimamizi na tathmini za miradi
ya barabara kwani wananchi hao wanaweze kuwa walinzi wa barabara hizo ili zidumu
na zitumike kwa malengo yaliyokusudiwa.
Dkt. Kone amewashauri
watendaji kuhakikisha fedha za ukarabati, ujenzi na ufuatiliaji wa miradi ya
barabara zinawekewa vipaumbele kwa wakala wa barabara Mkoa na Mamlaka za
Serikali za Mitaa ili maeneo muhimu yaweze kuhudimiwa.
Ameongeza kuwa ni
vizuri sasa kuandaa na kupanga maeneo zitakapopita barabara za michepuko ili kuepuka tatizo la
msongamano wa magari kwakuwa Mji wa Singida unakua kwa haraka na vyombo vya
usafiri vinaongezeka.
Kwa upande wao wajumbe
wa bodi hiyo kutoka Wilaya mpya ya Mkalama wameilalamikia wilaya ya Iramba kushindwa kusimamia miradi ya barabara
ipasavyo iliyo sainiwa mapema kabla ya kuundwa kwa halmashauri hiyo.
Mkuu wa Wilaya hiyo
Edward Ole Lenga amesema taarifa iliyoandaliwa na Wilaya ya Iramba haikuendana
na hali halisi ya miradi ya barabara zilizopo wilayani humo, ambazo mikatabaka
yake ilisainiwa na Wilaya ya Iramba.
Ole Lenga amesema
maazimio ya kikao kilichopita cha bodi ya barabara kiliazimia kuunda tume ya
kutathimini miardi ya barabara iliyosainiwa na Wilaya ya Iramba lakini badala
yake azimio hilo halijatekelezwa.
Kutokana na hoja hiyo
Dkt. Kone ameamuru uangaliwe uwezekano wa utaratibu wa kuvunja mikataba ya
barabara za Wilaya ya Mkalama iliyosainiwa na Wilaya ya Iramba awali.
Wajumbe wa Bodi ya Barabara wakifuatilia kikao hicho.
No comments:
Post a Comment