Thursday, April 11, 2024

SALAMU ZA POLE

Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe. Halima Dendego ametoa salamu za pole kwa ndugu, jamaa na marafiki waliopoteza ndugu zao kufutia ajali ya basi iliyoua watu Kumi (10) na wengine Sita (6) kujeruhiwa katika kijiji cha Malendi Wilayani Iramba.

 Ajali hiyo ilitokea majira ya saa 11 alfajiri (Aprili 10, 2024) ikihusisha basi la kampuni ya Lujiga ambalo lilikuwa linatokea Dar es Saalam kwenda Mwanza baada ya dereva wa basi hilo kushindwa kumudu basi hilo na kugonga lori kwa nyuma lililokuwa limeegeshwa kando ya barabara kutokana na mvua iliyokuwa inanyesha na hali ya ukungu.

 “Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya vifo vilivyotokana na ajali hiyo na Mwenyezi Mungu azilaze roho za ndugu zetu hawa mahali pema peponi Amina na awaponye majeruhi haraka ili waweze kurejea kwenye majukumu yao ya kila siku” Ameeleza Mhe. Dendego

Kufutia ajali hiyo, Mkuu wa Mkoa huo amevitaka vyombo vya ulinzi na usalama kuimarisha usimamizi wa sheria na ukaguzi wa mara kwa mara ili kuepusha ajali zinazoweza kuepukika.




No comments:

Post a Comment